Wenzako wanahonga vitu vya thamani, wewe unahonga bia

Wenzako wanahonga vitu vya thamani, wewe unahonga bia

ligera

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
2,646
Reaction score
1,173
Ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama dunia nzima tutaukataa .Kila mwanaume anahonga au alishawahi kuhonga katika katika historia ya maisha yake.

Kilichonifanya niandike thread hii leo ni kituko nilichokutana nacho bar niliyokuwa nakunywa hapa dodoma carnival . Mlevi mmoja baada ya kulewa mapombe yake kumwambia kijana mmoja aliyekuwa anakunywa na kisichana chake kwamba,

"Wenzako wanahonga wilaya wewe anahonga bia huko ni kuonyesha udhaifu ndugu." Watu wote tuliokuwa kwenye bar hiyo tulicheka sana kwani tulijua maana ya dongo hilo la chapombe. Yule kijana aliyetupiwa dongo hilo akajitutumua naye akajibu, " hajakusikia mhusika mpigie simu ".

Hawa walevi kweli nimeamini wakati mwingine wanakuwa na akili zao na kwamba si kila mlevi network inakuwa imekata .
Nikabaki najiuliza sisi tulio zoea kuhonga misimbazi sijui itakuwaje maana sasa huo msemo ndio msemo wa mujini ulioibuka wiki hii. Itabidi tujikakamue tuongeze dau kwa maana huo msemo umekuja kutudhalilisha wanaume tusiokuwa na kipato.
 
Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake na suala la kuhonga hata kama umehonga voucher ya mia 250 wote wahongaji
 
Dah!kweli hamfuatilii ngoja niwawekee picha afu mtafute wenyewe kapewa wilaya gani.
 

Attachments

  • 1424497385158.jpg
    1424497385158.jpg
    52.3 KB · Views: 497
Ukweli kabisa.
watu wanafaidi
 

Attachments

  • 1424498310349.jpg
    1424498310349.jpg
    78.2 KB · Views: 364
Watanzania bhana. Ila kama hizi picha zinazozagaa mitandaoni ni za kweli, basi kweli mkulu anafaudu aisee.
 
Back
Top Bottom