Wenyeviti wa mitaa watishia kujiuzulu

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
WENYEVITI wa Serikali za mitaa nchini wametishia kujiuzulu nyadhifa zao kama Serikali itaendelea na msimamo wake wa kuwanyang’anya mihuri ambayo wamedai kuwa ni vitendea kazi vyao.

Kutokana na hilo, wamemwomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, kutoa kauli kuhusu hatua hiyo ya kuwanyang’anya mihuri.

Msimamo huo waliutoa jana katika mkutano wao uliofanyika Dar es Salaam. Pia walitoa saa 24 kwa Katibu Mkuu Tamisemi, Mussa Iyombe, kuwaomba radhi kutokana na barua yake aliyoiandika Novemba 30, mwaka jana.

Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa wenyeviti hao kutoka Manispaa ya Kinondoni, Juma Uloleulole alisema: “Tunatoa siku saba kwa wakurugenzi wote walioandika barua kwa watendaji wa kata na Jeshi la Polisi kuwataka watupokonye mihuri watuombe radhi.

“Wakikaidi maazimo yetu tutajizulu nchi nzima na uchaguzi uandaliwe upya,” alisema Uloleulole.

Aidha Uloleulole ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kijitonyama kwa tiketi ya Chadema, alisema wanawaomba wenyeviti wa Serikali za mitaa nchini nzima kuunga mkono hoja hiyo kwani kitendo cha kunyang’anywa mihuri ni udhalilishwaji kwao.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Madale, Kata ya Wazo, Gratian Mbelwa, alisema mihuri hiyo hawakuvunja ghala la Manispaa ya Kinondoni bali walipewa kama vitendea kazi.
 
Wanang'ang'ania mihuri kwa kuwa kuna kula,hamna lolote,tunawajua hao.Mimi nawashangaa sana,kwa kuwa walipogombea walijua kwamba hiyo kazi ni ya kujitegemea, ndiyo maana wanatakiwa kuwa na shuhuli zao zingine.
WENYEVITI wa Serikali za mitaa nchini wametishia kujiuzulu nyadhifa zao kama Serikali itaendelea na msimamo wake wa kuwanyang’anya mihuri ambayo wamedai kuwa ni vitendea kazi vyao.
Kutokana na hilo, wamemwomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, kutoa kauli kuhusu hatua hiyo ya kuwanyang’anya mihuri.

Msimamo huo waliutoa jana katika mkutano wao uliofanyika Dar es Salaam. Pia walitoa saa 24 kwa Katibu Mkuu Tamisemi, Mussa Iyombe, kuwaomba radhi kutokana na barua yake aliyoiandika Novemba 30, mwaka jana.

Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa wenyeviti hao kutoka Manispaa ya Kinondoni, Juma Uloleulole alisema: “Tunatoa siku saba kwa wakurugenzi wote walioandika barua kwa watendaji wa kata na Jeshi la Polisi kuwataka watupokonye mihuri watuombe radhi.

“Wakikaidi maazimo yetu tutajizulu nchi nzima na uchaguzi uandaliwe upya,” alisema Uloleulole.

Aidha Uloleulole ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kijitonyama kwa tiketi ya Chadema, alisema wanawaomba wenyeviti wa Serikali za mitaa nchini nzima kuunga mkono hoja hiyo kwani kitendo cha kunyang’anywa mihuri ni udhalilishwaji kwao.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Madale, Kata ya Wazo, Gratian Mbelwa, alisema mihuri hiyo hawakuvunja ghala la Manispaa ya Kinondoni bali walipewa kama vitendea kazi.
 
Kama hawataki kuiachia chongeni mipya ya muundo mwingine muwape hao watendaji,then msiitambue mihuri ya zamani tuone kama wataitumia. Ila buku buku za mihuri tamu...
 
Wanang'ang'ania mihuri kwa kuwa kuna kula,hamna lolote,tunawajua hao.Mimi nawashangaa sana,kwa kuwa walipogombea walijua kwamba hiyo kazi ni ya kujitegemea, ndiyo maana wanatakiwa kuwa na shuhuli zao zingine.[/QU
UTAKAPOPATWA NA TATIZO LA KUPATA BARUA YA MWenyekiti kwa haraka na ukakuta yuko kwenye hizo hughuli nyingine utaona umuhimu wa angalao abakie ofisini na kuendeea kupata visenti viwili vya kukutayarishia nyaraka husika na bila mhuri ni bure. TUSISHABIKIE TU. kwa vile kuna mtendaji wapewe hiyo mihuri maana wapo ofisini siu zote za kazi
 
kiukweli hawawezi kufanya kitu kama hiko ila wanatishia tu ili waonekane kama wapo hata kama siri-kali imewakosea
 
Aisee! Hawa wenyeviti wa serikali na baadhi ya wajumbe wa nyumba kumi kumi ni watu wa ajabu sana.
Kuna mdogo wangu alifarakana na mkewe wakaenda kupatanishwa kwa mjumbe wa nyumba kumi kumi.
Mjumbe akatoa ushauri eti kwa kuwa Mke anaonekana kasononeka sana na Mume bado anaonekana ana hasira anashauri Mke alale kwake (Mjumbe) mpaka asubuhi ili hasira ziwapoe. Mke akawa anaafikiana na wazo la mjumbe.
Kilichofuata jamaa alitaka kushusha kipondo kwa wote. Kumbe yule mjumbe tabia yake ndio ilikuwa hiyo. Halafu anagegeda wake za watu.
 
Hawa wenyeviti wa mitaa wengi wao ni matapeli; wa mijini kazi yao kudhulumu viwanja vya wajane na wa vijijini kazi yao kuuza mashamba ya watu!!! Ni sahihi kabisa kuwany'ang'anya hiyo mihuri kwani wao sio watendaji!!!

Juu ya hayo kazi ya mwenyekiti wa mtaa ni huduma kwa jamii na wala sio full time job ya hata kudai mishahara. Ingefaa pia katika sheria ya serikali ya mitaa ianishwe kuwa wenyeviti na wajumbe wa mitaa ni lazima wawe wakazi na wenye kumiliki nyumba kwenye mitaa wanayohudumia; nasema hivyo kwa sababu utakuta sehemu nyingine wenyeviti na wajumbe wa mtaa ni walinzi wa makazi ya watu na hivyo hutumia wadhifa wao kushiriki katika uhalifu katika maeneo hayo ambayo ni wajumbe lakini they do not own any property hapo!!!
Concrete example ya hili ni kule Mbezi beach wajumbe wengi wa serikali za mitaa ni walinzi wa viwanja vya watu ambao ni absentee landlords; hawalipwi mishahara na wenye viwanja hivyo huingia kwenye nafasi za ujumbe kama njia ya kuweza kufanikisha maisha yao ikiwemo kushirikiana na wahalifu!!! Kumbukeni yule mama kutoka nchi jirani aliyekuwa anasakwa na serikali ya marekani kuhusiana na biashara ya madawa ya kulevya alikuwa amejificha kule Mbezi Beach 'A"!!! Uhalifu unaondelea huko Mbezi beach hufanikishwa na ushiriki wa hawa wajumbe wa serikali za mitaa!!
 
Back
Top Bottom