Nimesikia jana kuwa Mwenyekiti wa mtaa wetu amepita na kutoa taarifa kwa kila nyumba kwa ajili ya kufika ofisi ya mtaa ili kuchukua vyandarua vinne kwa kila kaya. Haya ndio mambo ya uchaguzi au kutokomeza malaria?

Ndugu yangu kachukue vyandarua hivyo kwa niaba ya familia yako. Acha kuweka siasa kila mahali. Huo mpango wa vyandarua upo kwa muda sasa na ni matokeo ya zile ziara za Bush.
Pia lazima ujue huyo mwenyekiti wa mtaa mmemchagua wenyewe. Kama hawafai au anahonga vyandarua basi uamuzi uko kwenu nyie wenyewe na wala sio hapa JF.
Kama huvitaki hivyo vyandarua, endelea na mizunguko yako, achia wanaovitaka wafaidi.
Mwakatundu kwa nini hatukugawiwa vyandarua hivyo baada ya Bush kuanzisha mpango huo? Kwa nini tugawiwe sasa hivi miezi michache kabla ya uchaguzi. Kwa kuelewa 'mbinu' zinazotumiwa na wanasiasa wetu nachelea kuamini kabisa kwamba jambo hili la kugawa vyandarua wakati huu lina element za kisiasa. Ni njia ya kutaka wananchi washukuru kwa kutoa kura zao!