Wenyeviti wa mitaa kugawa vyandarua vya mbu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenyeviti wa mitaa kugawa vyandarua vya mbu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bright, Apr 23, 2010.

 1. Bright

  Bright Member

  #1
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesikia jana kuwa Mwenyekiti wa mtaa wetu amepita na kutoa taarifa kwa kila nyumba kwa ajili ya kufika ofisi ya mtaa ili kuchukua vyandarua vinne kwa kila kaya. Haya ndio mambo ya uchaguzi au kutokomeza malaria?
   
 2. m

  mwakatundu Member

  #2
  Apr 23, 2010
  Joined: Jan 1, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu kachukue vyandarua hivyo kwa niaba ya familia yako. Acha kuweka siasa kila mahali. Huo mpango wa vyandarua upo kwa muda sasa na ni matokeo ya zile ziara za Bush.

  Pia lazima ujue huyo mwenyekiti wa mtaa mmemchagua wenyewe. Kama hawafai au anahonga vyandarua basi uamuzi uko kwenu nyie wenyewe na wala sio hapa JF.

  Kama huvitaki hivyo vyandarua, endelea na mizunguko yako, achia wanaovitaka wafaidi.
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  malaria haikubaliki....hima kachukue chandarua chenye dawa
   
 4. Bright

  Bright Member

  #4
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana wengine wakageuza hili zoezi kuwa deal la kupatia senti!
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwakatundu kwa nini hatukugawiwa vyandarua hivyo baada ya Bush kuanzisha mpango huo? Kwa nini tugawiwe sasa hivi miezi michache kabla ya uchaguzi. Kwa kuelewa 'mbinu' zinazotumiwa na wanasiasa wetu nachelea kuamini kabisa kwamba jambo hili la kugawa vyandarua wakati huu lina element za kisiasa. Ni njia ya kutaka wananchi washukuru kwa kutoa kura zao!
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  watanzania hatudanganyiki mwaka huu
   
Loading...