Wenye uzoefu tujuzeni ukweli.

Wenye uzoefu tujuzeni ukweli.

1. Imani moja ya dini.(hii inawaweka pamoja muda mwingi siku za mapumziko, inarahisisha malezi ya watoto, inaondoa feelings za kuona mwenzio anasikiliza zaidi viongozi wa dini kuliko wewe, etc)
2. Msipishane sana kielimu (na hasa asikuzidi). Mnaongea lugha moja kwenye mambo mengi na inaondoa complexities nyingi sana, including inferiority.
3. Msitofautiane sana kwenye mitazamo mbalimbali ya maisha.(hutengeneza sana negative feelings)
4.......
Naendelea kukumbuka zingine. Usidharau hizi muhimu sana.

Nashukuru sana kwa ushauri mzuri.
 
Angalia uchumi pia.Akikuzidi umatemate atakusumbua sana.Kikubwa ni DINI/IMANI NDICHO KITU CHA MSINGI KUZINGATIA.
 
Kila mmoja ana vigezo vyake set your own criterias zikuongoze kupata umtakaye
 
Habari zenu wanajamvi.
Me ni kijana wa kiume,bado sijaoa. Huwa najiuliza sana,nitatumia vigezo gani ili kumjua kuwa mwenza huyu atanifaa...nini cha kuzingatia kwa umakini ili kuwa na ndoa yenye amani,upendo na furaha?
Karibuni wenye uzoefu ktk ndoa zenu mtupe siri ya mafanikio yenu!

Yako mengi ila nitasema machache yatakayokusaidia iwapo utayazingatia:
1. Hakuna mwanadamu aliyekamilika (hata wewe hujakamilika hapo ulipo), hivyo sifa zozote utakazozilisti, kadri zinavyokuwa nyingi ndivyo itakavyokuwa ngumu kumpata aliyenazo nyingi/zote kati ya hizo.
2. Bainisha vigezo vya msingi; kwangu mimi: awe mwenye upendo wa kweli, si mbinafsi, asiwe mnafiki, awe mcha Mungu, awe anafahamu shughuli za msingi kama mwanamke ndani ya nyumba (mf kutunza nyumba, usafi, kupika, nk)
3. WEWE PIA ufahamu unavyopaswa kuwa kama mume na kisha kama baba (mf wewe ndiye mwenye jukumu la kuleta chakula nyumbani, kuhakikisha kuwa mna mahali pa kuishi, nk)
4. Jua namna ya kumpima katika vigezo hivyo: mfano, kama kila mkionana anakueleza mahitaji yake yanayohitaji pesa, mara 'mpenzi naomba ninunulie Samsung Galaxy nimeipenda, mara naomba ninunulie viatu pale Mariedo, nk ujue ana element ya ubinafsi.

Niishie hapo kwa sasa wadau wengine waendelee.

Nakutakia kila la kheri. Kumbuka kuwa mke mwema mtu hupewa na Mungu. ILA NA WEWE UJIANDAE KUWA MUME MWEMA.
 
Maana let say ungependa muwe mnatoka kwa sanaa i,e week hii mnaenda club na week zingine kuna mashindano ya miss Tanzania n.k. Sasa wewe mke uliechagua ni antisocial si utaiona ndoa chungu hapo. And vice versa mkeo labda ni social na wewe ni antisocial hapo itakula kwako . Ni vema kujua unataka ndoa ya aina gani, ziko ndoa za aina nyingi mno na si zote zinamfaa kila mtu hapana . Angalia interest yako, Muombe Mungu
 
Habari zenu wanajamvi.
Me ni kijana wa kiume,bado sijaoa. Huwa najiuliza sana,nitatumia vigezo gani ili kumjua kuwa mwenza huyu atanifaa...nini cha kuzingatia kwa umakini ili kuwa na ndoa yenye amani,upendo na furaha?
Karibuni wenye uzoefu ktk ndoa zenu mtupe siri ya mafanikio yenu!
Kunahizi herufi sita za mwanzo jatika alfabetiko oda, A, B, C, D, E na F

A = age, msitofautiane sana kwenye umri, tofauti ikiwa kubwa kuna tencency ya mmoja kujiona kama mzazi wa mwingine hivyo kumtriti mwenzie kama mwanae vile.

B = body structure. Hii ipo phisical zaidi. Jaribu kumfuta mwenye umbo unalopendelea naye awe anapenda umbo lako. Ingawa lazima ukubali kuwa maumbo huwa yanabadilika. Unaweza ukaowa kipetitit leo, lakini ukikipiga na misosi kinabongeka ghafra.

C = character zipoje? Hapa wengi huzificha. Lakini unaweza ukajuwa haiba yake kupitia mavazi, aina ya marafiki alionao, maeneo anayoyapenda, aina vyakula anavyopenda etc... Kwa mfano kila siku yeye ni kudai baga, kesho piza, keshokutwa hiki au kile cha hadhi hiyo. Mtu huyu unaweza ukapredict maisha anayoyapendelea .

D = displine. Displine ya mtu utaijua kwa namna ya maongezi au majibu yake kwenye maswali toka kwa wengine.

E = education background. Wenye elimu ndogo huwa wanatendensi ya kuamini kuwa mwenye elimu kubwa ndo anajuwa kila kitu na hivyo atakuachia kila kitu uamuwe wewe ndani ya nyumba. Huwa hawana ushauri hata kama anao atahofia elimu yake. Jitahidi muwe na elimu sawa au isiyopishana sana.

F = famili background. Wazee wa zamani walikuwa wanaangalia zaidi kama upande wa pili kuna magonjwa ya kurithi au la. Kwa mfano pumu, kifafa n.k.

Kuna familia ukiowa, juwa watahamia wote kwako. Na hasa kama una kauwezo kuliko wote katika familia uliyoowa. Jua mapema hilo na kama utakuwa tayari kwa hili we endelea, lakini usije ukabadirika baadaye kwani huwa yanaleta shida sana haya mambo ya kuowa mmoja halafu unahudumia wote.

Madewa, kazi ni kwako...
 
Imani pia ni kitu cha msingi kuzingatia. NI VYEMA KUOA MTU WA IMANI THE SAME WITH YOU ILI KUEPUSHA KUTOFAUTIANA KIIMANI.Mf. We mkristo unamwoa mwislam ati kisa mnapendana,leo mtaona vyema maana mapenzi bado ya moto but mkishazoeana shida inaanza.
Utamkuta mtu anasema ntabadili imani yangu nikufuate kwa ajili ya kuolewa au kuoa,JE AKISHAOA AU KUOLEWA,NINI KINAFUATA?
KUMBUKA ANAVYOMKANA MUNGU WA IMANI YAKE KWA AJILI YA KUOLEWA NAWE AU KUKUOA,VIVYO HIVYO NDIVYO ATAKAVYOKUKANA WEWE SIKU MOJA KWA AJILI YA KITU FULANI.
 
Kunahizi herufi sita za mwanzo jatika alfabetiko oda, A, B, C, D, E na F A = age, msitofautiane sana kwenye umri, tofauti ikiwa kubwa kuna tencency ya mmoja kujiona kama mzazi wa mwingine hivyo kumtriti mwenzie kama mwanae vile.B = body structure. Hii ipo phisical zaidi. Jaribu kumfuta mwenye umbo unalopendelea naye awe anapenda umbo lako. Ingawa lazima ukubali kuwa maumbo huwa yanabadilika. Unaweza ukaowa kipetitit leo, lakini ukikipiga na misosi kinabongeka ghafra.C = character zipoje? Hapa wengi huzificha. Lakini unaweza ukajuwa haiba yake kupitia mavazi, aina ya marafiki alionao, maeneo anayoyapenda, aina vyakula anavyopenda etc... Kwa mfano kila siku yeye ni kudai baga, kesho piza, keshokutwa hiki au kile cha hadhi hiyo. Mtu huyu unaweza ukapredict maisha anayoyapendelea .D = displine. Displine ya mtu utaijua kwa namna ya maongezi au majibu yake kwenye maswali toka kwa wengine. E = education background. Wenye elimu ndogo huwa wanatendensi ya kuamini kuwa mwenye elimu kubwa ndo anajuwa kila kitu na hivyo atakuachia kila kitu uamuwe wewe ndani ya nyumba. Huwa hawana ushauri hata kama anao atahofia elimu yake. Jitahidi muwe na elimu sawa au isiyopishana sana.F = famili background. Wazee wa zamani walikuwa wanaangalia zaidi kama upande wa pili kuna magonjwa ya kurithi au la. Kwa mfano pumu, kifafa n.k. Kuna familia ukiowa, juwa watahamia wote kwako. Na hasa kama una kauwezo kuliko wote katika familia uliyoowa. Jua mapema hilo na kama utakuwa tayari kwa hili we endelea, lakini usije ukabadirika baadaye kwani huwa yanaleta shida sana haya mambo ya kuowa mmoja halafu unahudumia wote.Madewa, kazi ni kwako...
Aisee, nimependa sana hii. Safi sana
 
Back
Top Bottom