Wenye uzoefu tujuzeni ukweli.

Wenye uzoefu tujuzeni ukweli.

Madewa

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Posts
467
Reaction score
192
Habari zenu wanajamvi.
Me ni kijana wa kiume,bado sijaoa. Huwa najiuliza sana,nitatumia vigezo gani ili kumjua kuwa mwenza huyu atanifaa...nini cha kuzingatia kwa umakini ili kuwa na ndoa yenye amani,upendo na furaha?
Karibuni wenye uzoefu ktk ndoa zenu mtupe siri ya mafanikio yenu!
 
Ukifika muda utavijua tu hivyo vigezo vya kuzingatia !!!
 
1) Vigezo unavyovitaka atakuwa navyo baadhi, hawezi kuwa navyo vyoote bse hujamuumba ww.

2) Atakuwa na tabia zinazovumilika.
 
aksante...vp suala la kuridhishana kimahaba,je,ni chanzo cha ndoa kudumu?
 
Binadamu hatutabiliki na nivigumu sana kujua tabia ya mtu pindi utakapoanzanae mahusiano coz wengine huwa they just pretend tu kama wanatabia nzuri lakini ukishamuoa tu utajuta kwa hiyo mitabia yake.
 
Ni kweli,je nini suluhisho lake?
 
Habari zenu wanajamvi.
Me ni kijana wa kiume,bado sijaoa. Huwa najiuliza sana,nitatumia vigezo gani ili kumjua kuwa mwenza huyu atanifaa...nini cha kuzingatia kwa umakini ili kuwa na ndoa yenye amani,upendo na furaha?
Karibuni wenye uzoefu ktk ndoa zenu mtupe siri ya mafanikio yenu!

Una mpenzi?
 
aksante...vp suala la kuridhishana kimahaba,je,ni chanzo cha ndoa kudumu?

Tunatofautiana ktk kuridhika baina ya wanandoa, cha msingi ni kuelimishana akuridhishe vp, na kukubali mapungufu ya mwenzako.
 
Na vp pale unakuta mwenzako hapendelei kufanya mapenzi...
 
Ndiyo ninaye...
Kama unaye mpenzi sasa tunaweza kuendelea.

Kila mtu huwa na vigezo vyake vya kumpata yule atakaye mfaa.

Mfano mimi napenda mwanamke anayemcha MUNGU, aliye serious muda mwingi, asiyependelea kuvaa nguo za aibu, asiye na makuu, anayependa kwenda na muda, mwenye talent za maisha.
 
kila jambo linaenda kwa hatua na umri, umri wako ungekuwa na maana kama ungeusema ili ijulikane ushauri upi utakufaa, isije kuwa ukapewa mihogo wakati stahili yako ni maziwa ya mama.
 
Mkuu...mawazo yako kama yangu...natamani sana kumpata mwanamke mwenye sifa izo...awe supportive n mothery....
 
kila jambo linaenda kwa hatua na umri, umri wako ungekuwa na maana kama ungeusema ili ijulikane ushauri upi utakufaa, isije kuwa ukapewa mihogo wakati stahili yako ni maziwa ya mama.

Nina miaka 25...
 
Vigezo vinategemea na interest yako. Wewe binafsi unataka mtu wa aina gani na ungependa ndoa yako iweje baada ya kujiuliza maswali hayo na kuyapa mjibu . Basi nenda mbele za Mungu muombe kwa kadili ya picha uliyoijenga ndani yako. Kumbuka fedha na dhahabu waweza kupewa na yeyote kama mzazi n.k lkn mke/mume mwema mtu hupewa na Bwana.
 
1. Imani moja ya dini.(hii inawaweka pamoja muda mwingi siku za mapumziko, inarahisisha malezi ya watoto, inaondoa feelings za kuona mwenzio anasikiliza zaidi viongozi wa dini kuliko wewe, etc)
2. Msipishane sana kielimu (na hasa asikuzidi). Mnaongea lugha moja kwenye mambo mengi na inaondoa complexities nyingi sana, including inferiority.
3. Msitofautiane sana kwenye mitazamo mbalimbali ya maisha.(hutengeneza sana negative feelings)
4.......
Naendelea kukumbuka zingine. Usidharau hizi muhimu sana.
 
Back
Top Bottom