Pistol
Senior Member
- Oct 13, 2015
- 194
- 86
WANANDOA wakongwe wanaoaminika kuwa na ndoa zenye umri mkubwa kuliko zote ndani ya Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wanatarajia kutunukiwa tuzo maalumu, Jumapili wiki hii katika tukio linalotarajia kukutanisha mamia ya wanandoa.
Tuzo hizo zitakazotolewa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu hilo, Eusebius Nzigilwa, zitakabidhiwa kwa wanafamilia watatu wanaoaminika kuwa ndoa zao ni kongwe kuliko nyingine, katika hafla ya wanandoa maarufu kama Kliniki ya Ndoa, itakayofanyika Msimbazi Centre katika ukumbi wa Maranta.
Mmoja wa viongozi wanaoratibu tuzo hizo, Nolascus Mpota alisema katika tukio hilo lililoandaliwa na familia ya wanamaridhiano na kusimamiwa na Idara ya Kichungaji na Utume wa Familia ya Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wanandoa hao watapewa tuzo, kama moja ya kumbukumbu ya maadhimisho ya Mwaka wa Huruma ya Mungu.
“Tumepata uthibitisho wa ndoa yenye umri wa miaka 61, kutoka Parokia ya Chang’ombe na ile ya miaka 57 kutoka Parokia ya Oysterbay. Hata hivyo, tunasubiri uthibitisho wa ndoa yenye umri wa miaka 67 ambapo kwa sasa wanandoa hawa wakongwe wako Mahenge, walikokwenda wiki mbili tu zilizopita wakitokea Segerea walikokuwa wakiishi, na tunaamini huenda ndio ikawa ndoa kongwe kuliko nyingine zote jijini Dar es Salaam,” alisema Mpota.
Hata hivyo, alisema ikiwa wapo wanandoa waliodumu kwa miaka mingi zaidi ya wale waliokwishajitokeza, watawapokea na kujinyakulia tuzo hizo ambazo hakuzitaja ili kutoa nafasi ya kutangazwa siku hiyo.
Alisema katika kliniki hiyo, Nzigilwa atatoa baraka maalumu kwa wanandoa hao na wote watakaoshiriki na itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, na kutatolewa mada na wataalamu wabobevu katika masuala ya ndoa na malezi ya familia.
Alisema lengo kuu ni kuwakumbusha wanandoa juu ya umuhimu wa kutunza na kuheshimu maisha ya ndoa na kutambua baraka na huruma ya Mungu inavyowasaidia wanandoa na wanafamilia katika maisha yao “Ni siku ya kutoka “out” na mwenzako wa ndoa, kula na kunywa na wanandoa wengine, hivyo tunawakaribisha wanandoa.
Watakaopenda kushiriki wajiandikishe mapema Msimbazi Centre ofisi ya mapokezi na kulipa ada ya kiingilio ya Sh 25,000 kwa kila mtu,” alisema Mpota.
Chanzo: Habari Leo