Wenye miaka 40 hatuajiriki?

Gor

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,791
Reaction score
850
Kwanini kila tangazo la kazi hata za serikali inakuwa na kipengele cha umri kuwa "kuwa asiwe zaidi ya miaka 35" wakati serikali inajua kuwa sisi amboao tuko katika rika hilo walitukosesha elimu na wengine tumekuja kujisomesha wenyewe kwa mategemeo kuwa siku moja nitapata kazi lakini hali sivyo;

Utashangaa taasisi za umma,viongozi wakitoa masharti haya ya kipumbavu na kibaguzi.lakini cha kushangaza wao wanahama kazi kila siku!.

Hii nchi vipi?,

hakuna haki kabisa,watu hatuna lili wala lile,basi tupeni hata mkopo kama basi!,jamani hii nchi gani ambayo oppotunities zipo kwa kundi fulani tu.....heri uwe panya road,tumechoka!,unaomba kazi mpaka unashikwa na uchizi!

Nina amini baba au ndugu yangu angekuwa na nafasi huko nisingeteseka hivi ktk ardhi hii
.
 
Hata Sitti Mtemvu anakuzidi akili?

Kama 40 years ni kikwazo katika kupata kazi, chakachua umri kama Sitti Mtemvu.
 
Hata Sitti Mtemvu anakuzidi akili?

Kama 40 years ni kikwazo katika kupata kazi, chakachua umri kama Sitti Mtemvu.

Alichakachua ila ilibuma. Ukishaingia kwenye mfumo wa digital, basi tena! Ili uchakachue umri wazazi/walezi wako ndo walitakiwa kuwa 'smart' enzi hizo. Ukubwani kuchakachua ndo hayo ya Sitti Mtemvu.
 
Mtu bado miaka 10 ufikishe umri wa kustaafu,bado unalilia kuajiliwa.Kuna watu katika nchi hii ni mizigo toka utotoni hadi kifo.
 
Mmh na ww mpka miaka 40 huna kazi duh tena unalilia ajira
 
Mtu bado miaka 10 ufikishe umri wa kustaafu,bado unalilia kuajiliwa.Kuna watu katika nchi hii ni mizigo toka utotoni hadi kifo.
Hivi mnasomaga mnachoandika? Atastaafu vipi wakati hana kazi!

Ubaguzi wa umri hata mimi unanishangaza kwenye matangazo ya kazi, nchi nyingi hili ni kinyume na sheria unaruhusiwa kubagua kwa vigezo vya kazi inayotakiwa kufanyika tu.
 
Reactions: Gor

Siyo lazima ufanye kazi serikalini ndiyo utoke kimaisha mkuu.
 
Jaribu sekta binafsi siyo lazima serikalini.
 
Hivi mnasomaga mnachoandika? Atastaafu vipi wakati hana kazi!

Ubaguzi wa umri hata mimi unanishangaza kwenye matangazo ya kazi, nchi nyingi hili ni kinyume na sheria unaruhusiwa kubagua kwa vigezo vya kazi inayotakiwa kufanyika tu.

Ngoja nikugonge like
 
Guyz, maisha yanachangamoto nyingi sana kabla hatujaanza kucriticized kuhusu umri wa jamaa na kutokua na kazi,tufikirie je mpaka anafikisha umri huo alikua anafanya kitu gani? je ndo janga la ajira lilikua linamhusu miaka yote hiyo?.Kitu kinachoonekana kwa huyu mkubwa ni frastuation ye hafikirii kua sio lazima uajiriwe na serikari tu, kuna private company nazo anatakiwa kuzicheki, vilevile awe na Plan B yan kama ajira inasumbua acheki issue nyingine for the living. Ni hayo 2.
 
Kama huna kitu hata ukipewa nguruwe 10 bure huweizi kuwalisha
 
Reactions: Gor
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…