Wenye CCM Wasiogopwe

Nairobian

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
873
Reaction score
2,282
Kuna kundi wanajiita wenye CCM. Hawa ni watoto wa wakubwa wastaafu.

Wanaojiona kana kwamba chama ni mali yao. Nawasihi sana wote wanaoitakia mema Tanzania wawakemee hawa watu.

Hivi karibuni, Nape Nnauyr alisema wqzi kwamba chama kimerudi kwa wenyewe. Hao wenyewe ni wakina nani?

Nadhani tutafika pabaya kwenye Ukiritimba, majungu, Undugu kwenye Ajira, uonevu na takataka zote tukiwavumilia hawa watu wanaojiita wenye CCM. Ufisadi utatisha kwenye hili Taifa
 
Akina Kingai Mahita Coodluck, Jumanne ndio wenye CCM, na walio shikilia pumzi ya ccm, kuanzia juu ngazi ya mwenyekiti taifa hadi mjumbe wa shina bila kujali vyeo vyao ni viroboto Kama viroboto tuu.
 
Wanajitutumua tu hao CCM ni ya kila mtu.
 

Hata msipowavumilia mtafanyaje, maana wote nyie na wao mnategemea vyombo vya dola kufanya siasa, na mkijitenga mkaja nje hamna support ya umma, nyie na hao wanaojiita wenye CCM. Itabidi mbaki humo ndani muendelee kulogana na kufanyiana fitina humo humo, maana dola tu ndio mbeleko yenu.
 
Wanajitutumua tu hao CCM ni ya kila mtu.

Ndio wanavyowadanganya, lakini kiuhalisia ni tofauti, si unaona Mwinyi baba yake alikuwa rais, na sasa Kawa rais. Watoto wa viongozi wa CCM wana uhakika wa ajira nzuri, na nafasi za utawala tena wakiwa hawana uwezo kabisa. Nyie wengine ni kuwabebea briefcase ili mpate uteuzi.
 
Hahahahahahaha
 
hawa ni wahuni?
 
Kwani hujui kama CCM ina wenyewe?
Kama huamini, nenda kamuulize Bashiru akusimulie nini kilimkuta yeye na kilimkuta Magu.

Wewe jua tu, CCM ina wenyewe na wenyewe wanajijua.
 
Kipindi Cha jk hakukuwa na undugu kwenye ajira hilo unamsingizia. Ni jpm ndo alianza kuleta undugu kwenye ajira mbalimbali
 
 
CCM haijawahi kuwa na nafuu ni lazima ifurumushwe kwa udi na uvumba
 
Alikataa kufanya internship ila akajipa leseni alipokuwa Naibu wizara ya Afya , na pia alikataa kujiunga na JKT lakini leo ni Amiri jeshi huko ng'ambo , nyuzi za ushahidi wa mambo haya ziko humu humu jf
 
Nape na January wanajiona nchi ni yao
Ni nchi yao kweli kama kalemani na shughuli yote Ile katolewa akapewa mtoto wa wenyenchi na mipango yote Ile ya madili, mi naona wako sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…