GE2025 Wengine wasahaulika Mchujo Kamati Kuu CCM.

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
858
Reaction score
1,655
NYONGEZA YA MAJINA YA WATIA NIA WALIOTEULIWA
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotajwa katika taarifa hii, waliteuliwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, iliyoketi Jumatatu, tarehe 28 Julai 2025.
Majina yao yalisahauliwa kutangazwa katika orodha iliyotolewa mapema leo na kusomwa mbele ya waandishi wa habari. Kutokana na uteuzi huo wa awali, watakuwa sehemu ya walioteuliwa kushiriki katika zoezi la kura za maoni kwa nafasi za ubunge, kama ilivyoelezwa hapo chini ya kila jina la mhusika:

1. Ndugu KIJAKAZI YUNUS MOHAMMED:
Ameteuliwa Ubunge wa Viti Maalum, kundi la wanawake kupitia UWT Mkoa wa LINDI.

2. Dkt. NEEMA PETER MAJULE
Ameteuliwa Ubunge wa Viti Maalum kundi la wanawake kupitia UWT, Mkoa wa Dodoma.

3. Ndugu PATALI SHIDA PATALI
Ameteuliwa Ubunge, Jimbo la Mbeya vijijini

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…