Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Wengi wampongeza Magufuli uteuzi wa Ma-RC
Rais Dk John Magufuli.
UTEUZI wa wakuu wa mikoa uliofanywa na Rais John Magufuli juzi, umeonekana kuwaridhisha wengi kutokana na watu wa kada tofauti kupongeza wakisema umezingatia weledi, elimu, rika na historia ya uchapakazi ya wahusika.
Mh Makonda akila kiapo
Miongoni mwa waliozungumzia uteuzi huo wakisema unaendana na kasi ya utendaji wa Rais Magufuli, wamo wasomi, wanasiasa na watu wa kawaida. Lakini pia, baadhi ya wakuu wa mikoa ambao wameachwa kwenye uteuzi, hususani aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, wamekosoa wanaodhani uteuzi una kasoro wakisema kutokuwamo baadhi ya watu, hakumaanishi kuwa uteuzi una upungufu bali uko sahihi na unaendana na kasi ya Rais Magufuli.
Hata hivyo, upande wa wanaharakati wa masuala ya jinsia, wameonekana kutoridhishwa kwa kile kinachodaiwa ni kuwapo idadi ndogo ya wanawake. Kandoro: Uteuzi ni sahihi Wakati huo huo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amepongeza uteuzi na kusema hana kinyongo kwa kutopewa nafasi katika uteuzi huo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kandoro alisema kutopewa nafasi kwenye uteuzi huo hakumaanishi kuwa uteuzi una upungufu bali uko sahihi na wenye kuendana na kasi ya Rais Magufuli. Hata hivyo, Kandoro ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa waliopita, alionesha kutoridhishwa na baadhi ya kauli za watu wanaozungumzia uteuzi huo akisema hauna tija katika utendaji wa kiserikali.
“Watu wasiwe na mtazamo hasi kwani nafasi yoyote ya kuteuliwa mwisho wake kuna ukomo hivyo tutambue kuwa anayeteua ipo siku anatengua uteuzi huo, nimepokea vizuri na ikumbukwe kuwa uteuzi ni uteuzi tu,” alisisitiza. Kandoro aliwapongeza wakuu wa mikoa wapya na zamani waliobaki, akisema hana kinyongo na kutokuwamo kwenye safu kwa kuwa muda alioitumikia serikali ni mwingi hivyo anastahili kupumzika na kuwaachia wengine.... Soma zadi hapa: Wengi wampongeza Magufuli uteuzi wa Ma-RC