Wengi tunadhani ndoa ni tendo

njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
12,041
4,957
Baadhi yetu tumelelewa na kukutana na mazingira yaliyotufundisha hivyo kwa hiyo ndivyo tunavyoamini. Tunaamini kwamba tunapooa au kuolewa tunafanya hivyo ili kushiriki tendo la ndoa kama dhana ya kwanza.
Ni ki
tu gani kinachotokea basi pale ambapo haturidhiki na kuridhishwa kiunyumba na wake au waume zetu?
Ni kwamba huwa tunadhani au kuamini kwamba hapo ndoa haina maana na hivyo huwajengea chuki wenzetu na pengine kutoka nje ya ndoa zetu tukidhani tutapata nafuu. Wanajamvi hebu tujiulize je ni kweli dhana ya ndoa ni kufanya mapenzi? Jibu ni siyo kweli hata kidogo.

Hebu tujiulize tena baada ya kuoana na kuishi kwenye ndoa kwa muda fulani wake au waume zetu wakapata matatizo ya kimaradhi au ajali au mengine ambayo yatawafanya wasiweze kabisa kushiriki jambo hili tutafanyaje? Huenda jibu kwa wale wanaoamini kwamba ndoa maana yake ni kufanya mapenzi watasema kwamba watakwenda nje au kwa wanaume wataoa wake wengine. Huu ni ujinga mkubwa mno kwani tunaweza kufanya hivyo ikiwa ni wenzetu waliopata matatizo lakini kama ni sisi tutaona inavyoumiza.

Tendo la ndoa katika ndoa ni muhimu na kwa kiasi cha kutosha husaidia pia kuimarisha uhusiano. Lakini pale kunapokuwa na tatizo kwenye suala hilo ndipo hapo upendo unapopimwa kama ni wa dhati, bandia, au upendo wa kimradi. Kama upendo wetu ni wa dhati tutajitahidi kuangalia mazingira ambayo huenda yatawafanya hao wenzetu wawe kama walivyo. Tunapojadili kwa upendo udhaifu fulani ni wazi tutawapa wengine nguvu ya kujikagua na kuzidisha upendo kwetu.

Lakini tunapokuwa wakali na kulaumu au kuchukia na kulaani tutawafanya wenzetu wajione wanyonge na pia tutawafanya au kuwapa nafasi ya kuhalalisha kwamba huenda sisi tumetawaliwa sana na tamaa ya kimwili kuliko uwezo wa kufikiri kiasi kwamba linapotokea tatizo tunakuwa vichaa na hivyo uwezekano wa kutoka nje au kuvuruga ndoa ni mkubwa. tujifunze kufahamu na kukubali ukweli kwamba ndoa bora na imara hazifanywi hivyo na tendo la ndoa, bali hufanywa hivyo na wanandoa kusaidia kutatua kila tatizo linalotokea. Ni vizuri tukawa wazi kusema matatizo tunayohisi kwa wenzetu badala ya kuhisi tu na kudhani watayaona. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeshindwa jukumu letu la kupenda kwani tutakuwa tumejitazama wenyewe zaidi..
28749_494591033895953_1835195240_n.jpg

 

prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
168
tendo la ndoa ndo kila kitu kwani mimi nimetoka kwetu kufuata nini kwako kwani kwetu nilikua sili au kufanya mambo mengine amboyo yapo kwako na kwetu yapo tendo la ndoa ndo linadumisha ndoa mnyime mkeo unyumba uone weeeeeeeeee itakua balaaa
 

fazaa

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,985
1,007
tendo la ndoa ndo kila kitu kwani mimi nimetoka kwetu kufuata nini kwako kwani kwetu nilikua sili au kufanya mambo mengine amboyo yapo kwako na kwetu yapo tendo la ndoa ndo linadumisha ndoa mnyime mkeo unyumba uone weeeeeeeeee itakua balaaa
Kwa hio jamaa asipo kuchangamsha nao, unaomba urudi kwenu... safi sana :biggrin1:
 

prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
168
hicho ndo kinamtoa nyoka pangoni bwana alafu ulete masihara weeee heeee fazaa we acha 2
 

njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
12,041
4,957
tendo la ndoa ndo kila kitu kwani mimi nimetoka kwetu kufuata nini kwako kwani kwetu nilikua sili au kufanya mambo mengine amboyo yapo kwako na kwetu yapo tendo la ndoa ndo linadumisha ndoa mnyime mkeo unyumba uone weeeeeeeeee itakua balaaa

ikatokea mume wako akapata maradhi ya ghafla je vipi utaisaliti ndoa yako..?
 

Heart

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
2,674
1,693


ikatokea mume wako akapata maradhi ya ghafla je vipi utaisaliti ndoa yako..?

Ikitokea tu ngoma ikawa hainyanyuki kwa jinsi nilivyoyaelewa maelezo yake ndoa nayo itakuwa kushney...!
 

zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
250
kwa uelewa wangu mdogo wa ndoa ikitokea mmoja anamnyima mwenzie unyumba hiyo kesi huwa ni kubwa mno hata mahakama wanaweza kuvunja hiyo ndoa!
lakini suala la kukosa watoto halina tatizo saaaaana!
 

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,260
20,610
ndoa ingekuwa tendo la ndoa, nyumba nyingi sana zingeshavunjika.

Kuna ule mstari kwenye biblia unasema "kwa sababu ya tamaa ya mwili kila mtu awe na mke wake mwenyewe
Sasa hapo source si naniliu?Au we unasemaje?Nadhani bila ngono hakuna ndoa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom