Wengi mnaoa na kuolewa bila maandalizi, mnatimiza wajibu bila kuwa na nia ya dhati

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!
Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza Ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Alingo,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall.. Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?? Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi. Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako??? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi????-
Salute to the composer of this article...please
 
Tena ngumu kweli kweli ndoa usipo jikaza mbona unaachwa na kila mume mpaka unapewa ila kumbe Subra na uvumilivu
sifuri,na ukiwa na mdomo,kazi hufanyi unasubiri kuletewa unategemea K ndio mtaji,hapo ndio pabaya zaidii.....
 
Kila mara nasema Hakuna umuhimu wa kuoa,ikiwa unapata yote yanayopatikana ndoani hivi sasa.
 
Jamani kuishi na mtu maisha yote kugumu. Unalala naye, unakula naye, unashinda naye, kila unachofanya umshirikishe, n.k. Jamani kunaboa.
Umewahi kufikiria mwenza anweza kupata gonjwa lisilotibika kama kansa?
Au akapata ajali akapoteza mvuto wake wa awali? Au akapata tatizo litalompelekea kuanza kukoroma kqma simba jike, kuanza kukojoa kitandani. Jamani kqma unapata mgegedo kwa michepuko ni bora usiingie kwenye ndoa. Mwenza anaboa .

Kadiri umri unavyosonga unaona mwenzako anakinaisha mpk unataka kujinyonga au kumnyonga.
 
Back
Top Bottom