Well done ITV, Wizara ya elimu Zindukeni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Well done ITV, Wizara ya elimu Zindukeni!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Lekanjobe Kubinika, Feb 19, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapo nyuma kidogo nilileta thread hapa jamvini juu ya ufisadi wa walimu wa shule za msingi na sekondari Dar es Salaam, hakuna aliyechangia lakini wachache waliisoma.

  Nawapongeza IPP media kupitia ITV, jana nimeona kazi yao hewani usiku kwenye taarifa ya habari saa mbili yenye kurudiwa saa tano kasorobo usiku. Exactly nilichokielezea ndicho nao walichokitafiti, wakagundua na mengi zaidi na hata kuwaanika wahusika wakitoa mfano wa shule ya msingi Kunduchi iliyoko Tegeta. Hata mnyamaze vipi, Wizara ya elimu zindukeni! Otherwise itaeleweka kwamba ufisadi huo umepangwa na wizara ikiwatumia walimu wachache vichwa ngumu.

  Imefika mahala, mkuu wa shule anafanyiwa kiburi na walioko chini yake kwa madai ati ni amri kutoka juu. Juu ya wapi inayobypass mkuu wa shule husika? Akikaririwa na ITV live mwalimu Regina Simon anayeendesha mradi wa chekechea shuleni hapo alikiri kwamba kweli amekusanya zaidi ya milioni mbili kutoka kwa wazazi, lakini ati kwa jeuri anadai hawajibiki kwa mtu yeyote kuonyesha mapato na matumizi ya makusanyo hayo. Anatumia resources za serikali laikini hataki aguswe. Jeuri hiyo kampa nani kama sio Wizara na system zake? Mtoto wa kike anaweza kuendesha danguro nyumbani kwa baba yake na asiulizwe na mtu yeyote?

  ITV ilionyesha wazazi wanavyolalamika kwamba mia mbili inayodaiwa ya "Kwizi" kwa kila mwanafunzi alio nao wawili darasa la saba wisipopatikana watoto wanakataa kwenda shule na akakiri ni pesa nyingi mno kwa mtu asiye na kipato consistently. Walimu wanakusanya na kula. Hawatoi risiti na hata wanapotoa hizo risiti hazikaguliwi na yeyote, ni feki. Hata serikali ya mtaa ambayo ndiye mwangalizi wa shule hiyo walipoulizwa walikataa kujua uhalali wa michango hiyo.

  Ile ni shule moja, ITVC wangekwenda na shule nyingine na hata shule za upili tungepanuka mawazo zaidi. Lakini Elimu wako likizo, sielewi kama wapo nchini, nadhani kama wizara zingine zilivyo wanachangamkia shughuli zenye per diem, hawana morali na kifo cha elimu ya Taifa. Ni sawa na mchwa anayekula mti unaowahifadhi.

  Kero wanayoisababisha walimu pale Kunduchi ni ya kweli na ipo pale kwa miaka mingi. Niliwaambia hapa kwamba kwa mwanafunzi mmoja bila kutoka na mia tano kila siku shule inakuwa chungu kwake pale Kunduchi, mmeona wenyewe ITI mliojaliwa kupata kuona. Hata hizo queez wanazodai watoto walipie, mara chache husaishwa, tena watoto wanaandika kwenye madaftari ambayo lazima wajinunulie. Mia mbili ni za "chai na soda" za walimu hata kama mitihani itakuwapo. Hivi, continuous assessment ya watoto darasani sio sehemu ya wajibu wa mwalimu? Kwa nini wizara kama imeshindwa kudhibiti walimu wake isihalalishe malipo hayo yajulikane wazi na kutolewa risiti ya serikali?

  Nene mvifile hiro.
   
 2. Iramusm

  Iramusm JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 428
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  WaTz kila mahali 'tunafisadiwa"
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...