Weka Moyo wako huru

Weka Moyo wako huru

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
42,412
Reaction score
104,848
Iwapo tutaishi katika uhusiano wa karibu na Mungu, ni muhimu kuwa wepesi wa kusamehe. Kadri tunavyosamehe haraka ndivyo inakuwa rahisi kuishi kwa amani.

Inaturuhusu kukabiliana na shida hiyo kabla ikite mizizi katika hisia zetu wakati Uchungu utakuwa mgumu zaidi kutoka iwapo utakua una mizizi mirefu yenye nguvu ndani yetu.

Tunapomshikia mtu kifundo, hatumdhuru huyo mtu bali tunajidhuru sisi wenyewe. Kukosa kuwasamehe watu wengine hakuwabadilishi watu hao, lakini hutubadilisha sisi wenyewe na hutufanya tuwe na kisirani, uchungu, dhiki na hifanya ugumu wa watu kuwa karibu nasi.

Na kutokusamehe ni njia danganyifu ambayo kutuweka katika utumwa. Wakati mwingine tufikiri kwamba tunapolipiza kisasi kwamba tunajilinda kutokana na kudhuriwa tena, lakini hakuna mojawapo la ukweli.
Kutokusamehe kunaendelea kukudhuru na kukuzuia kuipata amani ya moyo.

Inawezekana tu kuwa na afya nzuri kihisia ukiachilia uchungu wote na kusamehe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom