Weekend story! BEN 10

After being an addict for so long i died inside! Nje nilikiwa naishi sawa ila ndani nilikuwa nishakufa kitambooo sanaaa! Na jamiii ishanifanyia mazishi siku nyingi sanaaa! Manaka machoni pa jamii mimi ni tejaaa tu! There was no point of getting better because the society was gonna hold that one fact against me forver! Ndo maana moyoni nishajifia kitambooo! At this point katika maisha yangu nilikuwa siogopi kifo kabisaaa! Kabisaa kabisaa!

Hata huku ulaya na mama watoto we were betting our lives by swinging ghost! Conning the mater of them all! Seriously hata mimi sikuwa na uhakika mimba ni ya ghost au mwenzie! And yet sikustushwa hata chembe what ghost will do is cappable of doing!

Nikizungumza na mzazi mwenzangu namwambia bwana tungoje tuone mwisho wake! Hasira yake ikiwaka sanaa nitamwambia niue mimi apoze mori akuache wewe! Not that many people will miss me anyways! Maisha yangu nimechezea chezea mwenyewe! After all i am considering suicide only sijapata ujasiriwa kufanikisha! Mmmmmh! Na yeye bibie anasisitiza promise me Ghost akija kuniua huku you will pull yourself together na kumlea huyu mtoto! Promise me Hans! Na mdogo wake atakezaliwa utamlea cause you oweme that! I never gave upon you MF to the end so lazima uwalee wote! Hali kiukweli msomaji ilikuwa tete!

Ghost anatuma pesa ontime! Tutake nini kisije! Bibie ananiambia Hans anza kutubu ndigu yangu! Viama vyetu haviko mbali! Bibie woga akaamua aanze kumtafuta Sam! Just incase akituua wote abakie mtu kuwalea watoto! Hali ilikuwa tete!

Mi na mzazi mwenzangu mapenzi yashafarikigi siku nyingi mnoo! Na kama kitu kilichokufa chochote huwezi kukirudisha kwenye uhai! We just had this bond, ndugu si ndugu,marafiki si marafiki tupo tupo tu! Ila hisia za kimahaba baina yetu hakunaaa hakunaaaa!

Toka nije huku siku abuse kabisaaa! I am trying ndugu msomaji to quit! Sema sikuchukuliakama mile stone maana hata mwenyewe sijiamini kabisaa! Kesho tu nawezakutindinganya mambo! Nikawa nafanya zangu gym hapo nyumbani si nipo ideal! Body likaanza kukubali! Still the stigma na saikolojia zilikuwa in ashes! There was no point! And i was still suicidal!

Nikiwa nasafisha safisha nje ya hapo kwetu, nika mnotice dada mmoja mkaliiiiii hatariiii! Kila asubuhi namchungulia anavaa suit zake classic, anaendesha gari yake classic! Kazuriiiii!! Yani kazuriii! Na kako vizuriii! Kibongo bongo ningejitutumua ila kiulaya ulaya sio rahisi!

Nikamshirikisha mama mtoto my new crush! Kama mlitegemea atakuwa msaada ndo kwanza akazidi kunikausha uzazi wooote! Analalamika mwenzangu una ma crush ilihali mimi chakula hakishuki kwa utapeli tunaomfanyia yule kiumbe fedhuliiii na bandiduuu kuliko wote! Namwambia its just a crush dont be a party pooper! Mara akaniambia mwambie tu na usiache part ya wewe ni drug addict and see how it goes! Kauli hio ikanitoa upepo wote wa koro! There is no point ndugu msomaji!

Siku nikawa nafyekaaa! Akaja kuniuliza kama naweza kumfyekea na bei ikoje! Alikuwa high high kama anachelewa! Nikamwambia poa tutaongea bei! Nilifyekaaaajeeeee! Kama hakuna kesho! Mpaka pool nililiasafisha! Yaani ngaringari!

Akarudi akafurahi! Akaniambia aniajiri kwa kazi hio kwa mshahara wa kawaida! Nikakubali! Niji keep tu busy! Ghost alikiwa anatutunza tuna tunzika! Hatupungukiwi na chochote! Mwanangu kama hajaenda shule nae anakuja pale kucheza mi nafanya kazi za watu!

Siongei sana! Lugha yenyewe gongana! Shule sikusoma! Kichwani hamsini majulio! Mdada anaonekana hata mama mtoto hampati kwa vyeti! Siku akaniuliza umesomea nini? Anajifarangua i know europe can be hard unaweza kuwa umesoma na usipate kazi nimpe vyeti anisaidiekutafuta kazi! Mimi namuelewa ila kumjibu sasa kimbembe!

Nikamuita mwanangu aje awe translator! Namwambia haya Linda mwambie Aunty baba hajasoma sababu kichwani zero brain! Linda kunistiri baba ake nasema baba hajasoma sababu Afrika alizaliwa kijijini sana hamna shule! Damu nzito ndugu msomaji! Akauliza how do you live then? Doesyour mom work? Akadakia no she sleeps all day! Moms boyfriend is very rich! He sends lots of money from Africa! We dont need to work like you! Mmmmmh! Mwana sina hapaa! Akasema tu ooooh! So your mom and da are divorced? Dogo akapiga long time ago! Nikamsemesha kiswahii! Dogo acha shobooo! Mimi baba yako ujue!

Nikampanga kabisaa! Dogo mimi yule Aunty nimempenda, nataka awe mama yako sawa! Ili tuendele kwenda sawa issue zangu za madawa ziminyiemwanangu si unajua pops is trying his best! Akasema poa sitomwambia! Nikaendelea na usafi wa lile eneo kama miezi mi 2 hivi! Linda akaona kama sifanyi ma move yenye akili! Akaanza visa! Akamualika yule dada nyumbani! Anamuomba kabisaa mama ake! Dont be pain in the a.ss be nice! Mi mama mtoto namjuaaaa hawezagi unafiki! Na mimi sikuona ni akili nikasema anyways! Ngoja tuone!

Dinner haikwe da vibaya sanaa! Mama mtoto alijitahidi kusurvive na miguno ya hapa na pale! Huyu bibie anaitwa Serwaa ni mghana! Ni real estate agent! Alikuwa very nice! Na mwanagu alijitahii kunizibia gapes! Serwaa akamuuliza mama mtoto why did you 2 break up! Balaa ndo lilipoanzia! Akasema hakukuwa na sababu ya kuendelea! Nianzie wapi? Which part? Where i triedto mudder him? Or i served jail time for attempted mudder, orthe serial cheattings! Serwaa akamuwahi maybe you shouldnt start at al!

Kama kuniua ashanimalizaaaa! Alimuacha na maswali mengi sanaaa! Akaaga akaondoka zake! Ndugu msomaji kama unategemea tiffu lilifuatia wala hujakosea! Ila sio mimi wa sasa! Nikamuita tu kiutu uzima.

Nikamwambia kwanza naomba nikuombe msamaha kwa kukutoa kwa Sam! Perharphs nisingekutoa kuleusingepitia yote hayana niingekuharibia maisha! Naomba unisamehe kwa yote! Hakujibu kitu sasa sielewi alikubaliana au lipingana na hii hoja! Pili naomba nikuombe radhi tena kwa kuwa mzigo wa miba kwako! Kuwa dead beat dady, good for nothing! Mpaka unafanya mambo ya hatari kutuokoa mimi na mwanangu! Sina cha kukulipa! Akanyamaza!

Nikakandamiza lakini why dont you want me to go out with Serwa? Bado unanipenda? Hapana! Una hisia na mimi hapana? Hivo vyako visaaaa! Kweli nakwambia wewe mwanamke! Akasonyaaaaa!

Akasema mimi sina shida wewe kutoka na mwanamke yoyote ila sio Serwa! Akamaliza! Nikamuuliza wewe ulivotoka na Ghost nisingekuwa na shida ungetoka na mwanaume yoyote ila sioGhost! Lakini if he made youhappy iwas happy for you! Why cant you do the same!

Akasonyaa tenaaa! Hansa hunaa akili mbwa wewe! Kwa akili yako mimi kabisaa na majanga yangu nione wivu unatifua papa gani? Aaaah subutuuuuuu! Mimi nakuonea huruma! Serwaa sio size yako! Unakuwa mpanaaa kama kibao cha chapati ukiamua yako jpkama haya! Ukiyatindinganya utarudi kwenye addiction upyaaaa afu mimi ndo wa kuhangaika na wewe! Sitakiiiii! Hans niliokufanyia maishani mwako naweza kujivika cheoxha mama yako mzazi na nikiwa katika hii mamlaka nasema Serwa SIMTAKIIII! Tafuta msichana jinga jinga wa uwezo wako! Serwa anaweza kuwa hata CIA Ghost akakamatwa siwezi kiruhusu u risk maisha yetusababu ya Gapuchi! Na hio kazi ya usafi siitaki!

Kikao kikaishia hapo! Kesho nikampeleka mwangu shule na kuulizia kama kuna shuleya watu wazima! Nikaambiwa ipo night school! Nikajianikisha! Jioni namuaga mama mtoto naenda zangu shule! Mimi na shule tulivo vitu viwili tofauti sasa! Na mama mtoto anavonikatisha tamaa! Mwanangu ana ni support na Serwaa anani support! Japonimeacha kazi kwake bado tuna chat! Bahariabaharia tu!

Mambo aliokuwa anasema mama Linda yana mashiko! Kweli akijua mimi nabet drug addiction hawezi kunikubali! Sina kazi, sina mbele wala nyuma! Naelekea 40s! Pamoja na yote lazima nimle! Hata nikimkosa nimeonja!

Namtongoza kinge kidogo mwanangu n shule kikaanza kupanda! Ananiwekea uzibeeee! Namwambia toka nije huku ulaya sija do! Naumiaaa! Nionee huruma! Najua unanitaka! Protocal za nini maisha mafupi! Anazuga zuga! Jamaniiii! Sikati tamaaa!

Kumla pale kwake isingewezekana mwanagu mapepe sana!Atatuktisha! Nikalipia lodge mbali kidogo! Nikamwambia kama kubet tu ndouanaume njoo huku nikupige show! Nikajiwekeaakija poa, asipokuja poa!kama zali akaja! Nikamtafuna kisawasawa! Na hivi mwanaume suruali,msingi kiuno show moja ya kibabe! Heshima ikawepo!

Tofauti na nilivodhania atakuwa na tabia za kizungu kumbe walaaa! Mtotowa ki ghana ana maadili yote ya kiafrika! Kuniletea maji jikoni fresh! Nikasema wewe binti huna bahatiiii! Lazima nikutiemimba! Bongo sirudi ngoooo!

Mtotoana kazi nzuriana maweeee! Na mwanaume suruali napewama care! Nyumbani nikawa wa uhaba! Ma date kama yote! Mtoto kapagawa ananidolishia mpaka Accra huko kwa ndugu zake! Anawaambia Tanzania! Kanumbaa! Yes! Dimond platnumz! Yes!

Wasomaji wenyewe mnanijua kama mimi bahariaa! Nampanga mapemaaa kama umniridhia na hali yangu niko tayari kufunga ndoa na wewe! Anytime uko ready sema niko ready! Namvuruga kabisaaa! Mwanangu nae anatoa ushirikiano kwa mama wa kambo ulionyooka! Mama mtu dawa yake ndogo kuona Linda anafaidi pale kwa Serwa anapendwa na nini na yeye akajaaaa! Tukawa one big happy family! And i was trully happy after so long!

INAENDELEA KESHO SERIOUSLY
 
Nilivoanza kusoma nkajua unatupa brief fupi ya kilichojiri in your absence. Sa nkaona eti umekuwa addict, si najiuliza amarula imeanza lini kuwafanya watu wawe mateja?
 
Hii mimba ndugu msomaji imebakisha miezi mi 2 kamiliiii nijifungue! All this time na mawazo mchanganyiko! Sometimes i am certain and sure i should abort this baby! Its for the best anyways! Kwanza Ghost hajuikama na mimba! And KR doesnt care ni kama kafa tu! But wait Ghost anajua kabisaa nina mimba! Ndo maana hajaja huku kabisaa wala kuleta hila! Heis patiently waiting siku nitayojifungua ndo aje! Na akija there isno telling what he wont dokama mtoto sio wake!

Ndo maana ndugu msomaji naona bora niitoe tu! Na katika viumbe ambao sitakikuzaa nao kabisa kabisana ni abomination kuzaa nacho ni Ghost! His genes should die with him! Kitoto kitakuwa na roho ngumu sanaaa! Thinking mimi ndo nakileta hiko kiumbe duani ndugu msomaji usishange kusikia nimebana miguu leba mtoto kafia tumboni! I really am not so sure! Sijaridhia!

Apart from Ghost Linda mwanangu ana ni disapoint sanaa! She is very cruel to me! Ni mkatili mno mno! Mpaka kanifanya nifikie maamuzi watoto hawana shukrani kwa sisi wazazi! Ndo maana sioni umuhimu wakuongeza stress na blood pressure nyingine! Tuangalie tunazaa na nani! Linda is so stupid kama baba mtu! Kaenda kwa baba mtu jumla jumla! Ananikatisha tamaa sana! Nikimwambia kitu hatakiwi kufanya ana ni mock! Because you are such a good mom? Just to rub it in my face i am terrible mom! Monster mom ndo jina langu! Anamwambia Hans mimi ni Monster! And she is serious!

Kwenye diary kaandika I hate my mom! Kumpiga huku ulaya siweziiii! Nitafungwaaa! Nimekuwa mtumwa wake! Simwambiii kitu! Yalemauzembe yanguu yoteniliokuwa nafanya kumlea anayo kichwani kayahifadhi for negotiations purposes! Akitaka lake nikikataa ana jivictimise na kunikumbusha mapungufu yangu nakosa pa kutokea namuacha tu!

Her shopping expenses ni extravagant! Anaenda sleepovers, music concerts anachotakaaa! Nikimwamvia Hans ongea kidogo anasema mimi drug addict nasemajeee? Muache tu! Asiefunzwa na mama yake atafunzwa na dunia! Nauhakika ndugu msomaji Linda will amount to nothing in this life labda stripper au barmaid! Kichwani zero brain! Anapenda miziki! Baba yake mtupuuu! Na chamoto ananocho nipa sitamani kuzaaa kabisaa!

The only postive thing about hii mimba huenda ikawa ya KR! Yule nitamzalia hata watoto 10! Dunia inihurumie mtoto awe wa KR! Na atakuwa mtu safi sanaa! Ila dunia inavope da kunila kiboga hii asilimia kubwa toto ni la ghost!

I hate Serwaaaa! Sio kwamba kanikosea au vipi! First it is not fair for Hans to be happy again wakati bado mimi mambo yangu hayaendi! Sio kwamba namtaka Hans au vipi! Ila sio haki Hans ampate Serwaaa mwanamke mwenye kila kitu and they are happy together! Its like rubbing to my face that he is lucky and i aint shit! Na Serwaaa anampenda kweli! I jus cant stand them nor their love!

Linda pia ananifanya nimchukie Serwaaa! Anamuheshimu Serwaaa! Serwaa kama kamungu chake kadogo! Kila kitu lazima amuulize Serwaa! Mambo ya shule siambiwi ila Serwa anaambiwa, yeye ndo ananiambia mimi! Toto hili jamaniiii! Nampendaje Serwa kwa mfano? Chiu nimechanika mimi, mateso nimepata mimi, nilivoteseka kumleaaa leo anamuheshimu malay wa baba ake na kunidharau mimi nilie pata nae tabu! Watoto wengine tunazaa kutoa uchafu tumboni. Mi nawaangalia tu!

Nikajiwazia nikimpata Sam anaweza nipa msaada! Sawa nilivotoka jela hakunisaidia! Ila nijaribu tu! Mambo yao yatakuwa mazuri na Jenny! Nikaanza kumsaka facebook sikumpata! Nikamsaka Jane nikampata! Nikaanza kuchat nae mbali sanaaa! Sikutaka kumkurupua! Nikawa nachat nae sanaa! Aliniambia na Sam wako divorced ilakama namhitaji yeye anaweza kumpata atamwambia namtafuta!

Kuchat kuchat nikamsimulia Janet matatizo yangu! Akanihurumia! She was like an old sister! Akaniambia Moza vipi? Nikamwambia sijawasiliana nae kitambo! Tukawa tuna chat tu! Akaja Sweeden na mwanae! Alifikia 7 star hotel! Ana pesa kama zotteeee! Sahivi ananiambia pesa yake sio local ni international! Ana wafanyakazi wa 5 wanamlelea mwanae! Wawili manesi wenye vyeti vyao! Mmoja buttler professional! Wawili maids! Na wote ana fly nao business!

Hakukaa sana kwangu! Kuchafuuuuuu! Contaminated! Mwanae ana medical conditions! Nilimuelewa sanaa tu! Linda sasa! Ali ni torment sanaa! Kama ingekuwa amri yake pale pale na siku ileile angmfanya Janet mama yake mzazi!

Katika maongezi akaniambia Kylembona unaishi kama umekufa? Why? Najitetea i dont have a choice! Akaniambia we do have choices all the time! We only choose not to take them! Jamani msomaji niache tu! Tukaongea mengiiii! Na bwana wetu Ghost!

Akaniambia kwa sasa yeye hana bwana permanent na wala hatakiiii! Ana nunua top modelstu ana lala nao siku moja, anawapa cash afu basi! Hataki kuwekeza moyo kwa mtu mwingine! Na hatozaa tena! Akaniambia Sam yupo na ana mawee kiasi chake! Alimpa namba yangu! Anashangaa kwanini hajanipigia! Mwenyewe ndugu msomaji nilishangaaa na kuumia sanaaa rohoni! Mmasai ana roho mbaya sana yule!

Janet aliondoka! Ila tuna chat kila siku lazima aniambie vitu viwli vitatu vya kunichangamsha nibadilishe maisha! Baada ya Jjanet kuondoka biliwaza mambo mengi sanaaa!

Je ongekuwaje ningeolewana Sam katika udogo ule na kuzeeka nae! Au ningekomaa na Hans? Au ningekomaa na ghost? Au KR? Nikapata majibu kuwa dunia sio mbaya kwangu ila mwenyewe ni wenge tu! I am so selfish! Ndo maana sidumu na wanaume! Ila ndo basi tenaaa!

Nikawaza mimba nikajipa moyo nisikate tamaa! Kama Linda sio rizikilabda huyu takuja kunifuta machozi! I have failed every area in my life mpaka sasa but i wont fail generation! Damu yangu! Huyu ni wangu, mwanangu! Haijalishi baba ni nani! Bitampambania mpaka mwisho! Nitachokula atakula! Nitakapolala atalala! For once nitasimama kidete! Nitamngoja Ghost na nitapambana nae wima wima!

Nikapata ujasiri wa ajabu sanaaaa! Woga woteee ukaniisha! Nikaamua nabadilisha maisha yangu! Asubuhi nikaamka na nguvu mpya! Linda akaja kunitaarifu ana sleepover! Nikamwambia huendi! Akauliza kwanini? Toka lini mimi ndo msemaji? Nikamwambia nenda uone umenisahau! Akasema mama jua kuwa kuwa na mzazi teja na mzazi malaya mwenye mimba asiojua baba kwa mtoto wa umri wangu sio rahisi kabisaa! Naomba uniacheeee mama! My life is already a nightmare! Jioni sitolala kama nilivokwambia! Nikamwambia usilale hapa sasa ndo utajua umalaya wangu ni mkubwa kiasi ganiii na ndo utajua kama Hans ni baba ako mzazi kweli au nilimbambika! Akawazaaa! Akaenda shule!

Jioni akarudi! Saa moja akavaa nguo na kutaka kutoka nikamwambia rudi ndani? Akasonyaaaa! Akatoka! Nilimdaka barazani na kumshushia kipondo cha uhakika! Nilimburutia ndani kwanza! Nikafunga mlango! Cha moto alikipataaaa! Nilipanfisha sauti ya tv! Kelele zote zikaishia ndani! Ananiambia Monster Mom! Anapiga simu polisi nitafungwa jela! Niliporidhika! Nikamwambia simu ile pale piga polisi! Nakuruhusu! Bora nifungwe waru waseme umeharibika nikiwa jela! Sio niko hapahapa unajitia kufyatukaaaa! Piga niende jela, baba ako tejaaa, utapelejwa foster care za wazungu uwe unabakwa usiku ndo utajua umalaya ni nini! Hakupiga simu! Akaja kula nikamwambia hamna kula mpaka ujue mi nani na nimeteseka kiasi gani kukupa maisha mbwa wewe! Njaa ikizidi piga polisi wakuletee msosi!

Hans kama kawaida ni absenteee dad! Akaja akamwambia i snapped! Namfanyia domestic violence! Kidogo nimuue! Hans akajitia kupanic! Nikamwambia weeeeeee kama unataka niwe nakukorogea unga kwenye chai shoboka! Akajua sina mzaha!

Linda nilipambana nae wiki 2 non stop! Alinyooka mbona! Ni kipigo tu namshushia! Domestic violence kweli kweli! Akijitia nunda nimepasua Iphobe yake! Card ya bank nimebadilisha password! Kwanza simruhusu kuishika! Mommy monster kwelikweli! Nimechoma designer outfits zake! Akileta kiburi kina mcost! Alisalimu amri! Akawa na adabu! Nikampangia na kazi za ndani! Asipofanya simpi pesa!

Akahamia kwa Serwaa! Kule ndo akawa mfanyakazi! Serwaa hataki ujinga! Anamuachia kazi kama zote! Siku 3 akarudi mikono nyuma! Akaanzisha kwenye diary documentary ya surviving monster mom! Nikaitia kiberiti diary yenyewe! Sicheki na kima ndugu msomaji!

Akiamka ananisalimia shikamoo mama! Alianza kuniita Kyle! Akiita Kyle siitiki na moja ya valuable possessions zake iko hatarini! Mama ikakaa kwenye mdomo imenyooka! Nikajiona mshindi! Nikawaza kumbe najidharau tu! Linda nimemuwezaaa Ghost hawezi kunishinda!

Nikampigia simu! Tapeli la kimataifaaa! Anakutilia Kyle wangu! Mke wangu halali! Nikamchana tu live Ghost nina mimba! Akasema najuaaaa baby! Nikamwambia sina uhakika ni ya nani! Akanyamaza mda sanaa! Namjua! Nikaendelea! Whatever the case ni mwanangu na nitamlea!

Baada ya mda akasema unajifungua lini? Ghost ni ghost tu! Woga ukanirudia upyaaaa! Nikamwambia mwezi ujaoa! Akasema nakuja huko huko after 2 weeks na nitakaa mpaka ujifungue! Nikamuuliza kama mtoto sio wako? Aka kata simu!

Woga ulinirudi upyaaaaa! Nilichanganyikiwa upyaaaaa! Kwenye simu tu namsikia akitetemeka! Najitahidi kuongea na Hans hasomeki! Mghana ashampa nyama ya makalio hajisumbui na kilicho mbele yangu! 2 weeks ndugu msomaji!

Nikamuita Linda na kusemezana nae! Linda mwanangu sikuchukiii, wala sijawahi kukuchukia, na asilimia ya maamuzi yangu mengi ya makosa ni katika kujaribu kukupa maisha bora! You are the best thing that happened to me! Na ndo kitu cha thamani samani sanaaa kwangu! I will always love you! Akauliza mom are you leaving us? Are you dieing? Do you have cancer? Akaanza kupanic!

Nikamwambia no i dont have cancer! Wala sifi! Ni mongezo tu! Hii dunia! Just incase nikiondoka ila siondoki mwanangu! Akawahi mom dont leave me mom! I wanna go with you! I love you my momster mom! Please take me with you i dont wanna stay with dad and his girlfriend! Nikamwambia siondokiii na siweiz kukuacha wewe ndo maisha yangu! Ila just incase! Be nice to Serwaa and take care of your dad for me! Machozi yakaanza kunitoka na yeye machozi! Mjadala ukashindikana!

Usiku nikasikia anamfokea Hans, he doesnt care na mimi nataka kuwatoroka! Anamuhakikisha siwezi kuwatoroka! Anamwambia nauhakika mama anaondoka anatuacha! Hans anamwambia relax! Hata akiondoka lazima ni lazima aende na wewe Linda hawezi kukuacha! Anamwambia dad you are not listening! Muombe mama msamaha! Katukasiriia wote! And you should spend more time with us!

Hans akaja kuniuliza kama naondoka au haya mambo ya kuondoka yameanzia wapi? Nikamuuliza na tumbo hili niende wapi? Hakujali sana! Linda akaja kunichungulia mara 2 usiku! Asubuhi akawa hataki kwrnda shule nikaapia siondoki aende tu! Break akatoroka akanikuta! Nikamwambia Linda siondoki! Principle akapiga simu! Akaniuliza why Linda anahisi nitaondoka na kumuacha? Kuna matatizo nyumbani? Nikamwambia hamna! Na mimi nashangaa kwanini awaze hivo!

Baada ya siku 3 Linda akaanza kuwa kawaida na kuamini yalikuwa maongezi tu na siondoki! Jioni Ghost akapiga simu! Linda akamwambia she thinks i want to leave her na Hans hajua naenda wapi ila naondoka! Ghost akaniuliza nikamwambia nie de wapi? Kwa pesa ipi? Card nayotumia yake ya bank! Mtoto tu! Ghost was not convised alimuamini Linda zaidi! Navomjua baada ya hio simu anakata tiketi! Maana mda wooote ana visa ya EU! Ku confirm suspicion zangu Hans akarudi ghfla na kuniuliza nini kinae delea? Mbona nasikia Ghost anakuja kesho nisikwambie ila Linda ndo kaambiwa?

Nikamwambia mwache aje niko tayari kupambana nae! Akastukaaa! Akasema kesho nashinda hapa na wewe! Akija hio keshokutwa niwepo! Nikamwambia nishamwambia kila kitu! Anajua! Hans akasema nashinda hapa!

Asubuhi mwanangu kaenda shule, Hans kamuhakikishia anashinda na mimi! Nikamwambia naenda hospital! Akasema nakupeleka! Nikamwambia twende! Nimefika pale, nikaingia chooni na kumpigia Serwaa! Nikampanga leo birthday ya Hans tuna plan surprise birthday sasa fanya uwezalo umkeepvusy nipate mda wa kuandaaa hio party! Nikatoka! Serwaa akampigia simu kuna jambo urgent! Akamwambia hawezi kuja! Yupo na mimi hospital! Akanitumia sms! Nikamwambia mkomalie! Akamwambia usipokuja futa namba yangu! Akaniambia nikikuacha hapa uta mind! Nikamwambia hapana! Naenda sehemu fasta narudi! Nikamwambia sawa!

Katoa mguu na mimi nikaita tax airport moja kwa moja! Msafiri kafiri! Roho inaniuma ku!uacha mwanangu ila imebidi! Aluta continua!

ITAENDELEA!
 
Kichwani dear! Narumia nusu saa!
Asee pole , mi nikajua labda uwa unaandika at kwenye note pad kidogo kidogo then badae unkuja ku copy na ku oast. But mi ushaur wangu usiwe unatumia muda mwingi kutype just use five to eight min use iyo notepad yako ktk simu then save it badae uwe unadondosha ma vitu nasi uku maisha yatakua poa , jah bless kichwa na mikono yako
 
GOMA LILIIISHIA HAPA!
OKEY TWENDE SASA!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…