Nijuavyo ni kuwa UDSM kuna watu wa IT wenye uwezo wa kurekebisha muonekano wa tovuti yao, tatizo ni mazoea na priority.
Mazoea kwa maana kwamba nimewahi kushuhudia e-debate kati ya wanataaluma wakipinga kubadili tovuti ya UDSM kwa kigezo kwamba wameizoea na hawaoni umuhimu wa kuibadilisha. Mwisho wa debati ikaonekana hakuna haja ya kubadili na wale waliokuwa wamependekeza wakaambiwa kuna sehemu nyingi zinahitaji huduma yao kuziboresha na si tovuti hiyo pekee.
Kuhusu Priority nachelea kusema kwamba wanajumuiya hao hawaoni kama tovuti ni suala la kulipa kipaumbele kama masuala mengine ya upatikanaji wa vitendea kazi vya kufundishia na kusomea. Kumbuka, tangu limekuja suala la kuchangia gharama, Serikali kuu imepunguza sana mgawo wa fedha kwa UDSM kiasi kwamba wakati mwingine chuo kinashindwa kutimiza hata mahitaji muhimu kabisa kwa walimu na wafanyakazi wengine.
Labda tujadiliri namna ya kumaliza matatizo ya kifenda kwa chuo hiki kikongwe kabla ya kuangalia issue ya tovuti. Walimu pale wana matatizo kama vifaa vya kufundishia, vyumba vya madarasa vyenye ukubwa ambao hauendani na wingi wa wanafunzi, vitabu vya kiada na ziada, vyumba vya ofisi za walimu, na mengine mengi. Tukimaliza hili ndio tunaweza kuangalia hili la tovuti!!