WCB, wadau hamuwatendei haki Ben Pol, Belle 9 na wengineo

Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,872
1,206
Nimeliona hili na nikaona si mbaya kushea na wanajamii!!

Tanzania tumebarikiwa vipawa vya wanabongofleva vya kutosha na maridhawa kabisa!! Tumekuwa na wanamuziki wazuri hasa na kwa uchache nimewataja hapo juu kwenye head!! Kiufupi naona soko la muziki hapa kwetu Tanzania linaelekea kushikwa na wachache na kuwaacha WAKALI wengine wakipiga miayo au kuishi maisha ya chini tofauti na vipaji vyao!!

Diamond pekee tayari ana show nyingi mno hapa nchini na kimataifa hali ambayo si nzuri kwa wanabongofleva wengine!! Kuna wasanii hawapigi show mpaka kusubiri vitu kama FIESTA wakati wachache kila wiki ni wao tu majukwaani!! Ujio wa HARMONIZE na huyu RAYMOND unakuja kuongeza njaa kwa wanamuziki wetu wazuri kabisa kama Chegge, Matonya, Q chillah na weengi siwataji!!

Naona show nyingi sasa zitaelekezwa WCB kwa kuwa kila promota anataka pale!! Media, mitandao ya kijamii na karibia promo zote mjini zinazungumzia WCB kwa ziada!! Niwaombe wananchi wenzangu tuwathamini na hawa kina Mirror, Matonya, Belle 9 na weengi wanaojua kuimba!! Nawakubali sana WCB lakini ni lazma tuwajali wote wanaojua hii kazi ili nawao wafeel kipato cha jasho liwatokalo.

Ni hayo tu!!
 
Mwisho wa siku wasanii wote watataka wasainiewe WCB ili walau wapatize chochote kitu na wao...WCB miaka ya mbele kutakuja kuwa na jam sana ya wasanii pale,na media zote takribani Signature itayokuwa inasikika kila dakika ktk kila ngoma inayochezwa ni "waaaahsafiii"(wasaf record).
 
WCB hakutaweza kuwa na jam hata kidogo, maana WCB kwasasa ina wasanii watatu, mondi, harmo na Raymond.. Bado wasanii wawili tu ili watimie watano basii.. Jumla ya wasanii watakaokuwa chini ya wasafi ni watano tuu.. Na tarehe 2 June watamtambulisha rich mavoko kama msanii wao wanne, na msanii wa tano ataebakia atakuwa ni msanii wa kike
 
msanii wao wa kike walishasema ni queen darleen
 
WCB hakutaweza kuwa na jam hata kidogo, maana WCB kwasasa ina wasanii watatu, mondi, harmo na Raymond.. Bado wasanii wawili tu ili watimie watano basii.. Jumla ya wasanii watakaokuwa chini ya wasafi ni watano tuu.. Na tarehe 2 June watamtambulisha rich mavoko kama msanii wao wanne, na msanii wa tano ataebakia atakuwa ni msanii wa kike
Ya kweli hayo.
 
Muziki una pande mbili, kwanza kuujua muziki wenyewe na pili kulijua soko la muziki. Sasa wasanii wengine wanafeli upande wa soko la muziki. Huku kwenye soko ndiko ambako kunahitaji hawa watu tunaowaita mameneja. Unapomuona Diamond anakuwa na mameneja watatu ni kwa sababu anataka kuhakikisha soko la muziki halimuachi. Unaweza ukawa unajua kuimba vinzuri lakini ukakosa kung'ara kwa sababu ya kutojua soko la muziki.
 
Back
Top Bottom