WCB – RICH MAVOKO .....

WCB – RICH MAVOKO .....

Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2016
Posts
218
Reaction score
319
KOKORO- RICH MAVOKO FT DIAMOND , WIMBO BORA WCB WA WAKATI WOTE…HAITA TOKEA.

Habari zenu wandugu wa Jukwaa hili. Leo napenda kushea nanyimaoni yangu atika jukwaa hili juu ya Huyu Kijana Mavoko aka Messi wa Bongo flava. Watu wanamwite Messi si kwa ushabiki bali kwa kuwa amekuwa ni kachumbali kwa kila wimbo anao shirikishwa achilia mbali pale anapo imba mwenyewe. Tangu zamani Mavoko alionekana ndio tishio kwa Chibu pengine kuliko hata Kiba. Nasema hivyo wa kigezo kimoja kikubwa, Mavoko kama alivyo Mondi ni kwamba hana sauti kali ya kupanda juu (vocalization) hivyo kufanya auimbaji wake uwe wa kukatkata kwa kutaja maneno hasaka nap engine nusunusu au wa kuyaminya kitu ambacho hata Simba huwa anakifanya na ndio kimempa kujulikana na kupendwa zaidi kimataifa. Kwa kusema hayo ikubalike tu kuwa Messi ndio angeweza kushindana vyema na Simba kwa kuwa Ladha zao sinaendana, kama ukikosa ya Mondi basi unasikiliza Mavoko na kiu inaisha.

KOKORO.Mwaka 2016 mwishoni, kama sikosei ilikua ni Novemba. Hiki ni kipindi mbacho Taifa la Tanzania liliuwa limetoka katika uchaguzi mkuu ambao ulikuwa wa kihistotia kwa aina ya matukio na upinzani ulio tikisa. Si Tanzania tu bali hata nchi jirani zilitikiswa na kuwa na ushabiki kwa siasa za Bongo na hivyo basi Africa Mashariki na kati kuna kitu kilipwaya katika anga la burudani kwa takribani mwaka mmoja hivi. Baada ya kuisha kampeni zilizo wahusiaha wasanii kwa kiasi flani kuwa majukwaani na wana siasa ni dhahiri shahiri kuwa mnamo mwaka 2016 ilikuwa ni wakati muafaka wa watanzania kupata chakuala cha ubongo ili kuleta burudani inayo suuza nafsi kusindikiza michakato ya mkuu wetu wan chi ya utumbuaji majipu ambayo ndio iliteka vyombo vya habari kwa wakati huo.

Miezi michache nyuma kulitokea tukio nchini Kenya ambapo msanii Ali Kiba alitoa malalamiko kuwa Meneja wa ampinzani wate Mr.Salam alihusika na tukio la kuzimiwa kipaza na kuvuruka utumbuizaji wake. Tuhuma hizi zilijibiwa kwa kiasi falani na upande wa pili ingawa ilibaki dukuduku miongoni mwa wapenda burudani kutaka kujua kama kuna hujuma dhidi ya King Kiba.

Majuma machache mbele kulisikika maredioni kitu kipya sana na kilichi jaa kila aina ya ufundi. Awali ilikuwa aisikike sauti ya msanii toka Nigeria ambaye ni fundi wa midundo mitamu na tulivu sana kuwahi kutokea, huyo sio Miengine ni mzee wa kazi Mr. Tekno. Kulitokea namna na kuchelewa kukamilicha project-kokoro ndipo ikaamuliwa isiwe tabu, Mzee mwenye hati miliki ya Bongo falava Mr. Nasib bin J bin laden Baba tee Mr, Kivuruge akaamua kupasha mishuli na kutumbukia kiwajani huku akikuta gozi limetengwa ili abutue penarti. Huko Mjini Lagos mtaalamu wa midundo Alhaji Tekno akaona sio kesi akaendelea kujipanda na kuonesha usongo wake katika ngoma mbili kali ambazo zimekuwa game changer, alipo mpata mkali wa Bara Africa mr. Davido hapo ndipo akahamisha usongo wote katika ndoma matata iitwayo IF na haikupita muda akamalizia na FALL, kama hujawahi kuzisikia ngoma hizi najua labda utakua umetoka ICU leo au ndio umebandikwa masikio. Hizi ni ngoma ambazo zilipoza aina na mziki wa Kiafrica toka miziki ya kurukaruka na kudensi kwa maguvu na kuja kusakata IF I say I love yuuuu ndi ndi ndiiiii, Msema maalufu ni 30Billion for your account, yaani jamaa anawaza kuhonga Bilioni 30, huu ni utunzi wa Davido chini ya kichwa chenye usongo wa kuikosa Kokoro ya Mavoko. Baada ya IF utaona wasanii wote wameiga stlyle kwa kuanzia na Kiba- Sedude na Mondi –Eneka. Pia wapo wengi barani Africa wameiga stlyle. Pia huko duniani R.Kelly aliurudiia wimbo huo.

Turudi katika Kokoro, ubora wa wimbo huu unachangia kufanya Tekno ahusike vema kwa Davidio na IF na Fall.

Baada ya kukosekana Tekno Mondi aliingia na kufanya kitu cha ajabu sana. Kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa huu ndio wimbo wa Kwanza kushirikiana Hawa Magwiji wawili wa Bongo. Mondi hakutaka kufanya kitu cha levo ya chini, na utakubaliana na mimi kuwa hii ndiyo video ya kwanza ya Mavoko yenye ubora wa kimataifa kwa namna ilivyo amdaliwa lakini pia unamuona Mavoko anajaribu ku densi na watoto matata walio jazia chuza zao za wastani zisizo kera wala kukinai watazamaji wa ndani ya nchi na hata wazungu wapenda vimbaombao hapa wanakula ambianse bila kinyongo. Mwanzo anaonekana Messi akiwa katikati ya amabinti flani walio paka rangi ya fedha huku wakiwa wamechaguliwa kwa kigezo cha kuwa na dodo mbichi kifuani tena zile za saa sita. Mpaka hapo tu inakupa mzuka wa kundelea kukodoa. Mambo yanaendelea hukuna kule mara Gafla anaonekana Mondo mwenyewe akiwa anafanya vitu vyake. Sipendi nielezee sana kuhusu video hii ila tukija katika uimbaji tunaona Mavoko akiwa amebadilika dana,, anaimba maneno yasio ya msimu ambayo hayapitwi na wakati. Huku Mondi akiwa ametoa assist kimamilifu mapaka kubeba dancers wake akina Iyobo wote na kuwaleta kukamilisha Kokoro.

Huko mwisho kunatokea kibwagozo falni matata lakini kabla ya hapo mr. Mondi anatumia wimbo huo kueleza tukio la Kenya kwa Kiba, video inatiwa kama chenga flani kuashiria kuwa kuna mtu katikisa waya na hapo anatamka kwa kuuliza”Atakua Saalam nini?”Alafu kuna sauti ambayo nina ifanaisha nay a Queen Darleen dada yake Mondi ambaye ni rafiki wa zamani wa Kiba (kumbuka wimbo Wajua nakupenda ila unanihanda) hii kwa wahenga wenzanu lakini, Sauti inajibu “Mende zile” Hilo lilikuwa Dongo kwa Team Kiba. Binafsi mimi sikupenda kitendo cha wimbo huu kutumiwa na Mondi kumjibu kiba. “Kwanini asitoe nyimbo zake na amjibu Kiba atakavyo?” Naamini Mavoko Hana kokoso na Kiba.

Baada ya mipasho hiyo kunaisngia kibwagizo matata … Anadodoaa… anadodooaaa ….“Mond”anadodoka…. Yaani ni utamu mtupu ukisikia wiimbo huu. Wakati huo kunakuwa na vibinti falani vilivyo jaaliwa pahala pa kukalia vikiwa vina dodoka ila balaaa yaani mpaka video inaisha mtu unatama ni isiisha.

Huwezi kuzungumzia ubora na utamu wa wimbo huu bila kutoa pongezi kwa mtayarishaji @Abidady kwa namna alivyo fanya makufuru huku katika huu wimbo kutulizia stress. Ikumbukwe kuwa ni Abidaby alikuwa producer wa Kiba na baada ya kutengeneza Kokoro ya Mavoko, ilimuuma sana Kiba na kuamua kuhamia kwa Water, Hivyo utaona kuwa kuna matukio mengi yaliyo zunguka ngoma hii ya ajabu. Pia mtaalamu wa WCB wasafiiii…. Ayo Laizer… huyu Injinia wa WCB Mtoto wa Kigoma alie anzia haso zake kule Bujumbura na Warundi wanamkubuka na wanajilaumu kwani hawakutumia ipasavyo na sasa anafanya uinjinia wake pale WCB.

CHANGAMOTO. Wakati wimbo huu unatoka ni siku chache tu zilipita na Ghafla iliachiwa ngoma nyingine ambayo illeta upinzani mkubwa sana. Huu si tofauti na wimbo wa mwana Bongo Flava siye na makuu na aliye pambana vilivyo mpaka kutoboa. MUZIKI…. Wacha manemo weka Muziki…Nakumbuka siku hiyo nikiwa maeneo ya Kijitonyama nikamsikia mdada falani anampigia mwenzake aingie youtube kupakua wimbo matata wa Darassa, mwanzo sikutilia maanani sana kwakuwa sikuwa nimeona miandaoni kama kuna ingizo jipya mjini lakini ile shauku ya Yule binti ilinifanya niingie mtandaoni jioni na kutafuta Daraasa Muziki…. Duh… Kazi kwekweli nilikuta bonge la ngoma lenye burudani ya aina yake. Hii ni ngomamiliyo kuwa imajaza kila kona yaani kiokweli haikupwaya hata chembe. Watu wa upande wa pili mwa Kiba waona kama wamepata Mkombozi na kushabikia wimbo huu kwa kila aina ya mbwembwe. Hongera Darassa kwa nguvu kubwa na mafanikio hayo ila sidhani kama utaweza tena kufurukuta maana katika Muziki ulimaliza hazina yote na sidhani kama unajipya la kuzidi Muziki. Ingekuwa soka ningesema ustaafu na heshima yako maana kwa kazi ya Kuizima Kokoro hongera.

Baada ya kelele zote leo hii nimeisikiliza KoKoRo na kukubali kuwa huu wimbo ni mkubwa sana na ninatafakari kama ungekuwa wimbo wa Chibu basi ungempatia tuzo nyingi sana. Hongera RICHARD MAVOKO , MESSI wa Bongo Flava , kila pasi waya.

Kama unamaoni tafadhali changia kistaarabu.

“Siku nyingine nitaeleza jinsi Ali Kiba anavyo kosea kutumia ushindani wake kibiashara na hapo ninakusa kumuunga mkuno ingawa ngoma kama Mack Muga wangu ni wimbo wa ilele na nimawaidha” “ Kiba hana ubunifu na hana washauri wazuri”

“Mimi ni Shabiki wa wanamuziki wote lakini Mondi napenda Ubunifu wake kibiashara na jinsi anavyo jituma kujitangaza kimataifa”


KOKORO
 
Uko sahihi mkuu mondi ni mjasilia mali tofaut na mziki wake anao ufanya
 
Back
Top Bottom