WCB mshaurini boss wenu, akiendelea kumuwaza Kondeboy atapotea

Levels baby

JF-Expert Member
Sep 26, 2019
831
769
Naona boss Diamond hataki kukubaliana na ukweli kuwa Kondeboy kaondoka katika umiliki wake mpaka kutaka kutumia nguvu kubwa kutaka kumzima dogo huku amesahau kuwa alimfundisha njia zote ili arithi kiti chake, lakini alishindwa kucheza game ambayo ni fair kwa mfundishwaji.

Nikukumbushe unakumbuka safari yako ya mziki kwa kiasi kikubwa aliishikilia Ruge Mutahaba na akakufundisha njia zote bila kujua ipo siku utamkimbia na kutafuta chako mana mkataba wako nae uliiona unakunyonya, ndivyo ilitakiwa uucheze mchezo vizuri kuhusu kumsimamia Kondeboy.

Ilitakiwa umuongezee asilimia katika mapato ya show zake hata lebo kubwa duniani huwa zikiona msanii ana impact kubwa kwenye lebo zinamrekebishia mkataba ili nae anufaike zaidi kupitia jasho lake sasa wewe Kondeboy akapige show ya million 40 halafu mwisho wa siku achukue million 10.

Lingine najua kinachokuumiza ni yule bwana mdogo kuwa na akili za kujiongeza na impact yake uliona alivyoanzisha hiyo Zoom Production, lakini naona siku hizi kila mahali unamuweka karibu director Kenny ili asiondoke chini yako, sasa nikuambie dogo hata hiyo zoom kawaachia ila anahitaji amani nanyi ili mfanye kazi ya kulisukuma gurudumu la mziki.

Ila nawaonya mkiendelea kumuwaza bwana mdogo mtapotea maana nguvu aliyonayo nyuma yake sisi wengine tunaijua mtachemka vibaya mno.
 
Diehard fans wa Diamond sijui ni kwanini wamechukizwa sana na Kondeboy kutoka WCB..wamebaki kusubiria aanze kupauka kama Rich Mavoko..kitu ambacho hakiwezi kutokea

UNO audio tu tayari 1m+ stream on youtube..

Tuache uchawi..Diamond afanye kazi aendelee kuwa juu,na Harmonize naye aendelee kuwa juu na hata akimpita Diamond iwe ni ishu ya kawaida
 
Mnajitekenya na kucheka wenyewe,muda utaongea ukifika.#levels baby naona mmeamua kwenda Mtwara
Hamonenga nguvu aliyonayo tunaijua ndio maana unaona ma boss wake wa zamani wamepagawa mpaka ikatokea kaka mkubwa pindi kondeboy anatoa Uno alitaka nae atoe ngumu wakamshauri utapotea temana nae mpaka kampigia dogo Jux kuwa watoe ile yao mana lile la Jux kwaju kweli.

Haraf kaka kabaki na wakina Mwakyusa Wale wote hamna ubunifu na kujiongeza kama konde
 
Muda utaongea tu ,uzuri jamii forum thread huwaga hazifutwi,ila mnajitengenya na kucheka wenyewe,#levels baby naona mmeamua kwenda Mtwara.
 
Harmonize akimpita kwanza rayvanny ndo tutaamini kama anaweza kumpita diamond, note,hakuna msanii na hatotokea wa kumpita diamond.harmonize hata 1/3 tu ya diamond ajafika sembuse kumtetemesha?au kwa kuwa unajiita jina la kauli mbiu ya tigo fiesta levels baby(shoga),afu pia usimfananishe diamond (mbingu) na huyo ruge wako(ardhi) sawa.
 
Hamonenga nguvu aliyonayo tunaijua ndio maana unaona ma boss wake wa zamani wamepagawa mpaka ikatokea kaka mkubwa pindi kondeboy anatoa Uno alitaka nae atoe ngumu wakamshauri utapotea temana nae mpaka kampigia dogo Jux kuwa watoe ile yao mana lile la Jux kwaju kweli.

Haraf kaka kabaki na wakina Mwakyusa Wale wote hamna ubunifu na kujiongeza kama konde
Ahaaaaaaaaaaah acha kula bangi mbichi wewe kilaza wa mawingu fc,yaaani harmonize<rayvanny, ndo amtetemeshe diamond, diamond hakuna wa kumpoteza hata siku moja na haitatokea sawa.
 
Diehard fans wa Diamond sijui ni kwanini wamechukizwa sana na Kondeboy kutoka WCB..wamebaki kusubiria aanze kupauka kama Rich Mavoko..kitu ambacho hakiwezi kutokea

UNO audio tu tayari 1m+ stream on youtube..

Tuache uchawi..Diamond afanye kazi aendelee kuwa juu,na Harmonize naye aendelee kuwa juu na hata akimpita Diamond iwe ni ishu ya kawaida
Ahaaaaaaaaaaah kumbe ndo walewale yaani unaona haka na upepo ndo unampa kichwa huyo dogo daaaaaaah so sad
 
Back
Top Bottom