Wazungu wanaiogopa CCM

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kuna siku habari zilivuma kwamba Balozi wa Norway kaenda Unguja na kukutana wanasiasa wa huko bila ya idhini ya Serikali, baadaye Serikali ikatoa Waraka kwa Mabalozi wote kwamba marufuku kufanya shughuli bila ya kibali kesho yake Balozi na Ubalozi mzima wa Norway walianza kuhaha na kuiomba msamaha Serikali yetu kwamba hawatarudia tena!

Duh! Kweli nchi hii yetu inajiamini sana, nakumbuka kuna kipindi nilikuwa Kenya kwa shughuli, basi huko Balozi wa Marekani akiongea ni kama Raisi nchi anaongea, jeuri ya kupigwa waraka kama hapa tulivyofanya Wakenya hawana!
 
Tanzania ili mradi Rais anabadilika kila baada ya miaka 10
nchi wahisani hazina shida
hata Zimbabwe Mugabe mwenyewe kajiingiza mkenge
ingekuwa sera ni zile zile lakini Marais wamebadilika wasingewafanya kitu...


Wazungu deep down wanajua demokrasia karibu zoote duniani ni 'kiini macho'

chaguzi zinakuwa fixed hata huko makwao.....
 
ndio kila nchi ina sheria zake mbona sisi hatujawahi kusikia hata siku kuwa Balozi wa Tanzania ameenda Marekani na kutoa maamuzi ya jambo fulani wao kama nani hata watuingilie mambo yetu ya ndani haiwezekani jambo hilo ila lazima watii sheria za kila nchi kama tunavyo tii sisi Tanzania.
 
Back
Top Bottom