Wazungu wameichoka CCM, Wasituletee ya Libya



Huo uzalendo utapatikana wapi wakati wananchi wananyimwa haki zao. Hata sadam nae alikuwa kama shein tu. Ni wairak ndio waliomtoa madarakani sadam kwa kushirikiana na hao wazungu. Kama ni suala la kukosa uzalendo huo unaousemea wewe basi Mimi niko tayari kabisa kushirikiana kumuondoa nkuruzinza wa zanzibar.
 
Sawa sawa japo naombea sana amani Zanzibar kwani vurugu za eneo la kisiwa kama Zanzibar ni hatari sana
 
Usitujaze uwoga. CUF lazima itawale Zanzibar. Haturudi nyuma !!!!
 
Bifu la wazungu na CCM mbona limeanza zamani sana.Toka Nyerere aanze kupiga kelele za usawa kiuchumi na kuwasaidia ''magaidi'' kama kina Samora,Mandela ,Augustino Neto,Sam Nujoma, Amilcar Kabral ,Mugabe walishamuweka kwenye blackbook.Kimsingi alichokua anakifanya Nyerere ni kuwanyang'anya wazungu makoloni yao walioyatawala kwa miaka mingi. Wengi hawafahamu kuwa Msumbiji ilitawaliwa na Mreno kwa miaka 500. Nyerere na ''magaidi'' wake wa FRELIMO wakaamua kusitisha ulaji.Chuki yao haitaisha mpaka mwisho wa dunia.
 
Alafu hii tabia yà kudharau maoni yà muhimu kama yà mtoa Mada ikome. It's a very serious issue and the Government must be very alert. Solve Zanzibar conflict immediately before the "First World" nations uses it as a leverage for regime change.. ..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…