Wazungu ni Wazazi wetu sisi Waafrika (Kusini mwa sahara)!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Nimekuwa nikijuliza maswali mengi sana khs uhusiano wetu na Wazungu, nilichokuja kugundua ni kwamba sisi Waafrika (Kusini mwa Sahara) Wazungu ni kama wazazi wetu, wametulea tangu tukiwa watoto wametufundisha sema ,,ma" tukasema ,,ma", sema ,,ba" tukasema ,,ba" n.k kwa kifupi kila tunachokijua na kukiamini leo hii ni kile jtu ambacho Mzungu ametuambia na kutufundisha!

Na hapa itategemea Mzungu wa wapi, kama Mzazi wako alikuwa Mreno basi utajua tu khs yanayohusu Ureno na unafikiri Dunia nzima ni Ureno, kama ni Muingereza au Mfaransa vivyo hivyo, ndiyo maana utaona huku kwetu watu hawajui chochote nje ya kile Muingereza alichotufundisha na tunaamini kabisa kwamba anachofanya Muingereza ndiyo standard na kinafanyika Dunia nzima!
Kwa mfano sare za Shule ni mfumo wa Uingereza na Dunia nje ya Uingereza haijui sare za Shule lkn Mtanzania huwezi hata kuanza kujadiliana naye juu ya hili anaamini kabisa kwamba Mwanafunzi wa Shule lazima avae sare na hata kama hana uwezo ni bora akose Elimu lkn sare lazima awe nayo!

Ndiyo maana utaona kama walivyo wazazi wetu waliotuzaa, adui ya Muingereza ndiyo adui ya Mwafrika, kwa mfano WatanZania wengi kama vile Wakenya au watoto wengine wa kufikia wa Muingereza hawaipendi Ufaransa kwa kuwa tu Uingereza na Ufaransa hapo zamani walikuwa na ugomvi na walikuwa ni mahasimu, vivyo hivyo Waafrika watoto wa Mfaransa hawaipendi Uingereza lkn Ufaransa na Uingereza walisha move on na leo hii ni marafiki na wanashirikiana kwenye mambo mengi sana!

Hivyo ni ngumu sana kwa Muafrika kujinasua ktk kwa Wazungu kwa maana ndiyo waliotulea na hata bila ya kujua wote kwa namna moja au nyingine tumeathiriwa na malezi hayo ndiyo maana mpaka leo hii Kenya bado wanapeleka mitihani usahihishaji Uingereza ili iwekewe muhuri wa Mzazi wetu ndiyo iaminike, sisi mpaka leo hii nina uhakika mavazi yote ya kuanzia madiwani, Spika mpaka suti za raisi na Mawaziri tunatoa Uingereza, leo hii ukianzisha Kampuni hapa ya kutengeneza fimbo ya Spika Serikali haiwezi kununua ktk kwako au kushona nguo za Spika bado wataagiza ktk kwa Wazazi wetu!

Kuna mifano mingi sana nilikuwa Nzega huko ndani ndanii nikakutana na Kibao kimeandikwa Warning! heavy trucks turning ahead nikajiuliza ni kwanini kile kibao kisiandikwe kwa Kiswahili na kimewekwa na Halmashauri lkn majibu hakuna, ingawaje wenye uwezo wa kuelewa hicho kibao huko Nzega hawafiki hata asilimia 1 (1%) ya wakazi wa Mji huwo lkn Wazungu ambaye hata idadi yao haifiki hata laki Moja TZ nzima tunawawekea kibao kwa lugha yao!
 
Mpaka Leo tunaona fahari kuwaita watoto wetu majina kiingereza kuliko ya kiafica eti aya ya kiafirika tumeaminishwa yana mizimu.
 
Back
Top Bottom