Wazoefu wa interview karibu mnipe mbinu za kufaulu

Wazoefu wa interview karibu mnipe mbinu za kufaulu

Niambie Tu

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2022
Posts
280
Reaction score
727
Habari wakuu.

Hadi kufikia leo hii nimeshafanya interview kama tatu hakuna niliyopata.

Wiki hiki hii ninayo nyingine.

Hebu wanabodi mje mniambie nakosea wapi.

Maswali matatu niliyokutana nayo kote.

1.Tuambie wewe ni nani?

2.Endapo utakutana na mfanyakazi msumbufu kazini utafanyaje.?

3.Tukulipe Tsh ngapi ?

4.una familia au watoto?


Ni imani humu kuna watu wanahusika na maswala ya ajira na wanye uzoefu kwa interview msaada wakuu

Kada yangu ni Afya.
 
 
1: Jielezee kwa ufupi sana.
Ongea kuhusu jina lako, miaka yako, elimu yako, working experience. (muhimu sana hizo)

2: Kumuepuka kwa muda au kujenga mazoea nae ya kazi tuu pasipo kuwepo mazoea ya mambo binafsi hii itasaidia kutokuzoea sana mpaka kupitiliza.

3: Nilipwe kutokana na salary scale ya kampuni hii
 
1. Huu mtego usitaje historia yako, bali taja ubora wako kama vile muadilfu, mchapa kazi n.k
2. Utamshsuri, ilishindikana ripotia kwa kiongozi
3. Huu ni mtego pia, ila usitaje chini sana wala juu sana. Fanya tafiti wanalipa sh ngapi kwenye sehemu unapoomba kazi kwa nafasi unayotaka.
Asante sana Mkuu.
 
1: Jielezee kwa ufupi sana.
Ongea kuhusu jina lako, miaka yako, elimu yako, working experience. (muhimu sana hizo)

2: Kumuepuka kwa muda au kujenga mazoea nae ya kazi tuu pasipo kuwepo mazoea ya mambo binafsi hii itasaidia kutokuzoea sana mpaka kupitiliza.

3: Nilipwe kutokana na salary scale ya kampuni hii
Asante sana nakushukuru.
 
Habari wakuu.

Hadi kufikia leo hii nimeshafanya interview kama tatu hakuna niliyopata.

Wiki hiki hii ninayo nyingine.

Hebu wanabodi mje mniambie nakosea wapi.

Maswali matatu niliyokutana nayo kote.

1.Tuambie wewe ni nani?

2.Endapo utakutana na mfanyakazi msumbufu kazini utafanyaje.?

3.Tukulipe Tsh ngapi ?

Ni imani humu kuna watu wanahusika na maswala ya ajira na wanye uzoefu kwa interview msaada wakuu

Kada yangu ni Afya.
mtangulize Mungu mbele.
Mungu akubariki na akuinue
Amen.🙏
 
Wewe ni nani? Jina, Highest level of Education, work experience na majukumu (mbili mbili au kama ni moja ni sawa)

Ukikutana na mfanyakazi msumbufu? Si umewapa historia? Waweza sema hizo experience zimeimarisha communication talent so utawasiliana na mfanyakazi husika na kumwambia kampuni inachotarajia toka kwake.

Mshahara? Taja range unayojua watu wa hiyo kada wanalipwa.

Kwenye interview jitahidi kuonyesha usihadithie. So mfano hapo namba mbili waweza toa mfano kua nilipokua kampuni C kulikua na staff alikua A B C nikafanya A B C (Hata kama ni uongo ndo ujanja ujanja unaotajwa kwenye uzi fulani hivi.

Go get em
 
Habari wakuu.

Hadi kufikia leo hii nimeshafanya interview kama tatu hakuna niliyopata.

Wiki hiki hii ninayo nyingine.

Hebu wanabodi mje mniambie nakosea wapi.

Maswali matatu niliyokutana nayo kote.

1.Tuambie wewe ni nani?

2.Endapo utakutana na mfanyakazi msumbufu kazini utafanyaje.?

3.Tukulipe Tsh ngapi ?

Ni imani humu kuna watu wanahusika na maswala ya ajira na wanye uzoefu kwa interview msaada wakuu

Kada yangu ni Afya.
Vaa smart na kulingana na nature ya kazi unayoomba, akikisha umekusanya taarifa kuhusu kampuni husika na angalao unaijua vizuri, jibu maswali kwa usahihi na kujiamini, kabla ya kuingia kwenye chumba cha interview zima simu yako, mwisho kabisa utaulizwa kama una swali akikisha unawapiga angalao maswali mawili matatu ila yawe yanahusiana na masuala ya kampuni au kazi uliyoomba.
 
Mkuu naomba mbinu za kuitwa kwenye interview., mimi kwa haraka haraka nakumbuka nishafanya interview mbili za mahojiano. Mwenzangu upo 90! Ulikua unatumia mbinu gani kuweza kupenya unavyofanya applications
Japo sio mimi nimecomment.

Ila mimi mara zote ninahisi kwanini naitwa kwa interview.

Cv yangu nimeitengeneza vizuri sana yaani nilitumia siku nzima kusoma na kuunganisha cv za watu zaidi ya tatu.

So kuiboresha cv tu kumenisaidia.

Cha pili vyeti vyangu vyote nimevipa majina mfano John adam Certificate pdf ,john adam birth certificate,john adam Cv.

Umakini katika kutuma maombi kwenye email lazima uandike.kaujumbe kafupi kabla ya kuattach document.

Mfano

Dear Sir /Madam.

Good morning

Please let see credentials documents attached below and keep in consideration.
 
Vaa smart na kulingana na nature ya kazi unayoomba, akikisha umekusanya taarifa kuhusu kampuni husika na angalao unaijua vizuri, jibu maswali kwa usahihi na kujiamini, kabla ya kuingia kwenye chumba cha interview zima simu yako, mwisho kabisa utaulizwa kama una swali akikisha unawapiga angalao maswali mawili matatu ila yawe yanahusiana na masuala ya kampuni au kazi uliyoomba.
Hivi ukiwa hauna swali la kuuliza unajishusha credit
 
Mbna simple sana, na hapo kwenye kulipwa Bei gani wengi hua mnakosea au kilishana ujinga eti " as per govt scale" taja figure kabisa Ili wajue upo kikazi zaid nahukuja kuuza sura.
 
Hivi ukiwa hauna swali la kuuliza unajishusha credit
Ndio mkuu utaonekana haupo interested sana na kampuni husika jitahidi uulize chochote ukipewa nafasi ila yawe machache tu mawili yakizidi sana matatu mfano what are the greatest challenges facing your company?, what are the companies goals for upcomong years?, If I were hired for this role, what would you want me to achieve in my first month? n.k epuka kuuliza maswali personal sana mfano How much can I expect to earn during the first year?, do you have children n.k
 
Japo sio mimi nimecomment.

Ila mimi mara zote ninahisi kwanini naitwa kwa interview.

Cv yangu nimeitengeneza vizuri sana yaani nilitumia siku nzima kusoma na kuunganisha cv za watu zaidi ya tatu.

So kuiboresha cv tu kumenisaidia.

Cha pili vyeti vyangu vyote nimevipa majina mfano John adam Certificate pdf ,john adam birth certificate,john adam Cv.

Umakini katika kutuma maombi kwenye email lazima uandike.kaujumbe kafupi kabla ya kuattach document.

Mfano

Dear Sir /Madam.

Good morning

Please let see credentials documents attached below and keep in consideration.
Hahaha CV za watu watatu zimetoa moja ambayo ni yako 😂
 
Back
Top Bottom