Wazo: Uanzishaji wa benki ya Manii "sperm" duniani

Wazo: Uanzishaji wa benki ya Manii "sperm" duniani

Samwemgomba

Member
Joined
Mar 25, 2019
Posts
35
Reaction score
15
Habari zenyu bandugu wadanganyika?

Poleni na michakato na harakati za maisha ya kila hususan katika kipindi hiki cha harakati za uchaguzi mkuu wa madiwani wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Hiki ni kipindi ambacho angalau kuna kamzunguko kidogo wa fedha kuelekea uchumi wa kati ambapo harakati za uchaguzi zinaleta matumaini kwa waja! Bila shaka miamala inaongezeka sana wakati huu, ofa za vinywaji baridi na moto katika vijiwe vya kahawa, al kasusu na kwenye mabaa zimeongezeka tofauti na miezi michache, wauza kuku nao wanajiongezea kipato kutoka kwa watia nia wanaotekeleza maagizo ya kamati zao za ufundi kuelekea siku ya kilele ya uchaguzi ndani ya vyama na uchaguzi ili mradi kila mtu yuko katika nafasi ya kuingiza chochote! Wapo vijana wanachora picha za wagombea na kuwauzia kwa bei nzuri, wapambe na makuwadi wa wagombea ndio muda huu wa kumake chochote, yani angalau kila mtu yuko kwenye position nzuri ya kukutwa na mzunguko wa fedha.

Kiuhalisia kwa mtazamo wangu kama taifa tumekuwa na OMBWE na utawala na uongozi na kukosekana Watu mahsusi wa kuturudisha kwenye mstari kwa maana wengi wa wazee wetu hata wale ambao ni wasomi na wamewahi kushika nyadhifa za juu kabisa serikalini wamekaa kimya ama wanakuwa wanafiki, wazandiki na waoga kupindukia! Nchi nzima kimya ni Kusifia tu mpaka watu wanachupa mipaka na kumfananisha Kiongozi mkuu na Bwana Yesu Kristo! Nani atokee awe kama Mlezi na mshauri wa Taifa akemee, kukosoa na kushauri vyema kwa mana nchi hii haiongozwi na malaika bali ni wanadamu ambao wana madhaifu yao mengi tu.

Yapo maswali mengi sana kuhusu uhuru wa mihimili ya Nchi i.e Serikali, Mahakama na bunge, uhuru wa watu, utawala wa demokrasia na haki za binadamu etc. Nani wa kumfunga PAKA Kengele! Ushiriki wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Taifa katika siasa za nchi hii ukihusiana na Chama tawala ni jambo geni na linalokiuka sheria tangu tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa 1992! Nani akemee hili?

MAMBO HAYA NDIO YALIONIFIKIRISHA na kuona ipo haja ya KUANZISHWA kwa BENKI YA MANII DUNIANI ikiwa na lengo ya kuhifadhi mbegu za kiume kama inavyohifadhiwa damu kutolewa kwa watu fulani na kuhifadhiwa ili ije kutumika kwa watu wengine siku za Mbeleni! Sina uhakika kama wazo hili linawezakana au limeshafanyiwa kazi ila Hasira zimepelekea kuota ndoto hii.

Naamini kuwa vizazi vya binadamu wenye weledi, maarifa na akili nyingi, ushujaa na uthubutu huwa havitokei mara kwa mara! Kwa mfano, vizazi vya watu kama Mwl. NYERERE, Mandela, Kamwe Nkurumah, Malcomx, Martin Luther King, Cheguevala, Isac Newton, Lionel Messi, CR7, MARADONA na Pelle(mchawi mweusi) hivi ni miongoni tu mwa vizazi vya dhahabu katika nyanja tofauti za Maisha.

Kama wazo hili linawezakana isha kuwa too late kwa kina Mwl NYERERE na Nkuruma lakini hawa wakina Lionel Messi inawezekana kabisa zikachukuliwa sperms (manii yao) na kuhifadhiwa katika vyombo maalumu ili zije kupandikizwa miaka ya baadae kufanya Dunia isiishiwe na "extra ordinary peole" watu wajuvi hali itakayopelekea dunia isiwe sehemu salama ya kuishi.

Kwa yanayoendelea Tanzania naamini Mwl Nyerere angelikuwa HAI asingekuwa mfano wa mzee Mwinyi kutaka KATIBA iarishwe ili Mkulu aendelee kutawala kwa kipindi cha ahsante! "WITH"-what is the hell? Asingekaa kimya kama mzee Mkapa, Mwinyi na Kikwete.

Asingekubali mwanae Makongoro awe Rais kama ambavyo Mwinyi Jr anaenda kuapishwa bila kujali atashinda au laah!

Asingekubali mke wake mama Maria apewe UBUNGE wa kuteuliwa kama ambavyo mama Salma ameteuliwa! Mwl alikuwa tofauti sana, ilipaswa manii yake yahifadhiwe kwa ajili ta kuja kupata akina Nyerere wengine 2090 na 3090 huko.

Nisiwachoshe nafikiri nimeeleweka hii ndoto ilikuwa ya kutisha sana!
 
Hahahaha huyu makongoro pure product uwezo wake ukoje? Je artificial.... Watairudisha nyuma dunia maana watakuwa watu wakale

Hukuwaona wale watoto walokwama kisa CIVID-19 unajua wanapatikanaje!

CC. SALMA
Mama unagombea ubunge tunajua huna njaa unataka kutuwakilisha namna gani sisi wananchi ili tukupe ridhaa?
 
hahahaha huyu makongoro pure product uwezo wake ukoje? Je artificial.... Watairudisha nyuma dunia maana watakuwa watu w kale hukuwaona wale watoto walokwama kisa CIVID-19 unajua wanapatikanaje!
CC. SALMA
Mama unagombea ubunge tunajua huna njaa unataka kutuwakilisha namna gani sisi wananchi ili tukupe ridhaa?
Cha kuelewa hapo ni kuwa Golden Generation hutokea kila baada ya miaka mingi inaweza kuanzia hata kila baada ya miaka 100, madkongoro yupo within ya miaka 100 ya mwl that's why he was useless
 
Ni wazo fikirishi, ila kwa mfano wa Nyerere, kulikuwa na haja gani ya manii wakati watoto wake wapo na hakuna hata mmoja aliyefuata nyayo. Hivyo uthibitisho ulio wazi ni kuwa hata hizo manii haziwezi kutupa JK Nyerere mwingine.

Na pia ndio maana Mtikila aliondolewa kupisha huu ujinga wa enzi hizi, laiti naye angekuwa hai!
 
Ni wazo fikirishi, ila kwa mfano wa Nyerere, kulikuwa na haja gani ya manii wakati watoto wake wapo na hakuna hata mmoja aliyefuata nyayo. Hivyo uthibitisho ulio wazi ni kuwa hata hizo manii haziwezi kutupa JK Nyerere mwingine.

Na pia ndio maana Mtikila aliondolewa kupisha huu ujinga wa enzi hizi, laiti naye angekuwa hai!
Huwez jua kitanda hakizai haramu, familia zetu za Kiafrica kwenye watoto 10 wa baba mwenyew wanaweza kuwa 3, wengine amesaidiwa ila cha msingi KIZAZI CHA DHAHABU HAKITOKEI MARA KWA INAWEZA KUCHUKUA HATA MIAKA MUA MBILI IJAO
 
Duh, ndoto nyingine hizi!

Binafsi nimeielewa, wasiwasi wangu ni je jumbe kama hizi huwa zinawafikia na zikiwafikia huwa wanajifikiriaje kwa mfano?
Au ndo unafiki na kurithishana vinaanza kushika kasi.

Nawaza tu.
 
Duh, ndoto nyingine hizi!

Binafsi nimeielewa, wasiwasi wangu ni je jumbe kama hizi huwa zinawafikia na zikiwafikia huwa wanajifikiriaje kwa mfano...!!?
Au ndo unafiki na kurithishana vinaanza kushika kasi.

Nawaza tu.
Wako bize na kufuatilia tamthilia ya sultan na ma box ya pop corn yakiteketea
 
Back
Top Bottom