Sera ya elimu pamoja na mambo mengine ya kuendesha tasnia nzima ya elimu, leo mimi najikita zaidi katika kuangazia nguvu kazi, na hususani waalimu.
Nimejaribu kumwangalia huyu mtu anaeitwa mwalimu nimegundua kuwa ana mzigo mkubwa sana katika shughuli zake za kila siku.
Kabla sijatoa hoja yangu msingi ya leo, naomba nitoe angalau kwa muhtasari wajibu wa "teaching professional"- (walimu), ambao ni pamoja na kufundisha darasani, uangalizi wa tabia za wanafunzi(discpline), ushauri(consultation), upimaji wa maendeleo ya kitaaluma, kuandaa na kuratibu ufanyikaji wa mafunzo kwa vitendo(hapa zaidi kwa masomo ya sayansi).
Wazo langu sasa ili kuleta tija katika sekta hii ya elimu ni vema hayo majukumu nilitaja hapo juu yagawanywe na yafanywe na watu tofauti, kwa wazo langu ningependekeza mgawanyo uwe hivi, Mwalimu abaki na ufundishaji darasani, kushauri na kuangalia discipline ya wanafunzi. Lab technician yeye kazi yake kuandaa na kusimamia, kuratibu ufanyikaji wa practicals na kundi la tatu ni watu wa kupima maendeleo ya kitaaluma(Evaluators)-ambao kazi yao ni kutunga mitihani na kusahihisha mitihani hiyo na kutoa majibu.
Hawa Evaluator watakuwa na uhusiano mkubwa sana baraza la mitihani kwa hiyo wao pia watakuwa wanahusishwa na kwny kazi za baraza hilo.
Hata katika kusoma vyuoni wawepo watu wanaosomea katka upimaji zaidi katika vyuo vya waalimu!
Hili jambo linawezekana kabisa, mfano kwenye sekta ya afya ndo maana yupo daktari, yupo nurse na pia yupo mtaalam wa maabara, sasa kwa nini mwalimu alundikiwe kazi zote hizo na zote ni nzito kweli ukiangalia undani wake.
Najua serikali inaweza kuona ni gharama kubwa sana kuajiri watu wengi hivo katika idara moja lakini ni muhimu sana katika kuboresha elimu na hususani kumuondolea stress nyingi anazo kumbana nazo mwalimu kwa hali hii ya sasa!
NAKARIBISHA MAWAZO ZAIDI ILI KUBORESHA HII DHANA/HOJA YANGU.