Wazo binafsi: Je tuige serikali ya Nigeria kupiga marufuku kelele za nyumba za ibada?

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Serika ya Nigeria imefungia makanisa kadhaa kwa kushindwa kufunga vidhibiti sauti (sound proof) na kusababisha usumbufu wa kelele kwa wananchi. Uamzi huo unaihusu pia misikiti yote nchini humo.

Kwangu mimi hili ni wazo zuri serikali yetu hasa mawaziri wanaohusika na mazingira, afya na Tamisemi kuliiga na kulitungia sheria. Utakuta koni ya msikiti imeelekezwa dirisha la chumba ninacholala na wakianza adhana saa 10 usiku mi ni usumbufu mtupu. Au mikesha ya wenzetu kwa baadhi ya makanisa ni usumbufu usiku mzima.

Miji yetu imepangiliwa vibaya. Utakuta nyumba za ibada nyingi ziko kwenye makazi ya watu na kelele za ibada zao ni usumbufu mkubwa kwa jamii inayozunguka nyumba hizo za ibada.
 
Kwa misikiti alaumiwe Ali Hassan Mwinyi. Kwa makanisa alaumiwe mzee Mkapa. Suluhisho ni kuvaa uwendawazimu kuzifungia.
 
Pointless, baseless, worthless uzi usiokuwa na maana kbs !!
badala ya kufikiria maendeleo na kuboresha usafi mitaani na makazini tunatumia
uchokonozi.. ili tupate "KUVUTA na NIKUVUTE" !! time ya wananchi ni mali tusipoteze ovyo !!
mpk IkuluKwetu siyo wakati wa kulaumu tuangalie mbele....

Bavaria tafuteni cha maana....
 
Mtu anawaamsha waislam wenzie kwa makelele ambayo yanawaamsha na wapagani, kwa nini wasijiwekee alarm ya kuwakumbusha muda wa ibada????

Wapagani hawambughudhi yeyote katika waamini, Naunga mkono ipigwe marufuku kuwapigia kelele watu kwa kigezo cha ibada.
 
Hoja hiyo imeungwa mkono,wanaoikubali tuseme ndiyo......,ndiyoooooooooo!!
 
Back
Top Bottom