Waziri wa Ulinzi Ufaransa: Ulaya haitashiriki katika muungano wa baharini wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Waziri wa Ulinzi Ufaransa: Ulaya haitashiriki katika muungano wa baharini wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi
Aug 30, 2019 11:59 UTC
Florence Parly 
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa amesema kuwa, Umoja wa Ulaya hautashiriki katika muunano wa baharini unaoongozwa na Marekani katika Ghuba ya Uajemi.
Florence Parly amesema huko Helsinki kabla ya kuanza mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kwamba, nchi za bara hilo hazitashiriki katika operesheni za Marekani za kusindikiza meli za kibiashara katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa ametoa matamshi hayo kufuatilia jitihada zilizofeli za Rais Donald Trump wa Marekani za kutaka kuzishawishi nchi mbalimbali kujiunga na muungano wa baharini wa nchi hiyo katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
Kwa sasa ni Uingereza, utawala wa Kizayuni wa Israel na utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain pekee ndizo zilizotangaza kuwa tayari kujiunga na muungano huo wenye lengo la kuzidisha mashinikizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Baada ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei mwaka 2018, Marekani imekuwa ikifanya kila liwezekanalo kwa ajili ya kuibana na kuzidisha mashiniziko dhidi ya Iran. Katika mkondo huo, Washington imezidisha idadi ya majeshi yake katika eneo hilo na imekuwa ikifanya uchochezi dhidi ya Iran ikishirikiana na waitifaki wake kama Uingereza.
Hayo yote yanafanyika kwa kisingizio kisicho na msingi eti cha kulinda usalama wa safari za meli katika Ghuba ya Uajemi. Hata hivyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa, Iran na nchi za kanda hiyo ndizo zinazopaswa kusimamia na kulinda amani Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormuz.
 
Back
Top Bottom