Kumekuwa na Uzi mbalimbali humu JF zinazoonesha malalamiko mbalimbali ya jinsi bodi ya mikopo Elimu ya juu (HESLB) Kwa kushirikiana na maafisa utumishi kuingiza makato kwenye mishahara ya watumishi wa umma hata ambao hawajawahi kukopeshwa na HESLB ama wengine kumalizana na bodi miaka kadhaa iliyopita kupewa barua kama uthibitisho lakini HESLB imekuwa ikirudisha makato kimakosa na kuleta usumbufu mkubwa katika kufuatilia marekebisho yake.
Ukifika ofisini kwao kudai chako wanakuambia refund inajazwa online, ukijaza hata usitarajie kuipata kwa wakati kwangu mwezi wa pili sasa,hata online feedback haioneshi kama wanafuatilia, ukipiga simu hawapokei yaan ni kero juu ya kero.
Makato haya yanaingizwa kimakosa na maafisa utumishi Kwa kushirikiana na maafisa wa HESLB cha kujiuliza, kwanini hawa maafisa utumishi hawafanyi mawasiliano na wafanyakazi hali wana taarifa zote za watumishi, wana namba za simu, email hata Kwa kufahamiana.
Kwa kweli wiki hii nzima sijaenda kazin nafuatilia Hela yangu ya sikukuu wateja wangu watasubiri mpaka nitakapofanikisha.
Ninaomba Waziri wetu watumishi atoe maelekezo Kwa maafisa utumishi kuhusu kadhia hii tunayoipata lakini pia afanye mawasiliano na waziri wa Elimu au maafisa wa HESLB watafute namna nyingine ya kupata wadaiwa.