Waziri wa Nishati anapolingopea Taifa

Waziri wa Nishati anapolingopea Taifa

Nsabhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2011
Posts
1,093
Reaction score
162
Ndugu wanaJF nimekuwa nikifuatulia kwa karibu sana jinsi waziri wa Nishati prof. Muhongo anapolidangaya taifa letu kuwa hakuna mgao wa umeme. Je anafanya hivyo kwa maslahi ya nani wakati nchi ipo gizani?

Leo nimefuatilia na kugundua kuwa zaidi ya mikoa kumi haina umeme. Hivi huyu ni prof kweli au ni Prof kama vile wale wanaojiita hivyo? Namuomba aache mara moja kulidanganya taifa maana ulimwengu wa sasa si kama wa miaka ya arobaini na saba aliyozaliwa yeye!

Kama ataendelea na uongo wake wanaJF tuitishe maandamano ya kudai umeme na pia kumtaka waziri Muhongo achie ofisi ya umma maana bado hatujafikia kuongozwa na waziri muongo.
 
Kulikuwa na uzi hapa jukwaani uliokuwa unaongelea mgao wa umeme asubuhi ya leo ila cha ajabu umeondolewa!

Sasa sijui ni maagizo ya serikali au nini kilitokea mimi sina jibu!

Na huu uzi nao sijui kama utadumu.
 
Charambe na chamazi huko mbagala hakuna umeme toka asubuhi hadi sasa
 
hii wizara sijui wampe gamba gani ataweza kama msosi wa muhogo ameshindwa na mikwala yote
 
Hakuna mgao, kukatika kwa umeme ni kwa sababu ya miundo mbinu mibovu. Serikali haukuwekeza kwenye miundo mbinu kwa muda mrefu na sasa tunalipa. Hii sekta ni kama shamba la bibi, Net Solution walikuja hapa wakala hadi kutapika, na walichokifanya ni kupiga rangi majengo tu!
 
Mi huwa nashangaa wanaposema eti ukatikaji wa umeme unatokana na MATENGENEZO. Nasangaa maana matengenezo gani yanafanyika leo, kesho hayafanyiki, keshokutwa yanafanyika mtondogoo hayafanyiki! Huku kwetu juzi usiku kulikua hamna umeme ukarudi alfajiri, ukakatika tena jana mchana umerudi leo asubuhi kisha ukakatika mchana umerudi jioni hii.. Tabu tupu
 
Usishangae ndugu yangu mbona inajulikana serikali ya Jakaya ni serikali ya viongozi waongo kila mmoja wao anadanganya, wanashindana kwa kusema uongo
 
Ndugu wanajf nimekuwa nikifuatulia kwa karibu sana jinsi waziri wa nishati prof. muhongo anapolidangaya taifa letu kuwa hakuna mgao wa umeme. Je anafanya hivyo kwa maslahi ya nani wakati nchi ipo gizani? Leo nimefuatilia na kugundua kuwa zaidi ya mikoa kumi haina umeme. Hivi huyu ni prof kweli au ni prof kama vile wale wanaojiita hivyo? Namuomba aache mara moja kulidanganya taifa maana ulimwengu wa sasa si kama wa miaka ya arobaini na saba aliyozaliwa yeye! Kama ataendelea na uongo wake wanajf tuitishe maandamano ya kudai umeme na pia kumtaka waziri muhongo achie ofisi ya umma maana bado hatujafikia kuongozwa na waziri muongo.
Umepiga Simu ya emergency ya TANESCO wakakuelezaje. Wapigie Kama hujafanya hivyo
 
Dar si salama tena, umeme, maji, foleni na kila aina ya bughudha, jamani karibuni mikoani, Songea huku umeme 24/7.
 
Dar si salama tena, umeme, maji, foleni na kila aina ya bughudha, jamani karibuni mikoani, Songea huku umeme 24/7.

Hakuna usalama wowote songea. Hatuchekan mkuu maana huo umeme sio wa grid so yale mafuta machafu yakikosekana huwa mnamaliza hata wiki bila umeme. Cha msingi ni kudai umeme kwa watanzania wote bila kujal.ni dar au tunduru
 
Umesomeka mkuu but for now tuna-enjoy.
 
Poleni sana nduguzanguni.

Habari kama hizi zinaua moyo sana hata kama mtu unakusudia kurudi nyumbani.

Labda kama una mpango wa kupigana vita juu kabisa zinaweza kukutia moto kwamba utarudi kuzikabili.

Otherwise frustrations tu.
 
Hapa Mwanza hakuna umeme tangia jana asuuhi hadi saizi
 
Haraka ya nini banaaa!? Fanya utafiti wa kina kabla ya kuamua kutia timu usije ukajuta bure na kulia kilio cha mbwa mdomo juu.

Poleni sana nduguzanguni.

Habari kama hizi zinaua moyo sana hata kama mtu unakusudia kurudi nyumbani.

Labda kama una mpango wa kupigana vita juu kabisa zinaweza kukutia moto kwamba utarudi kuzikabili.

Otherwise frustrations tu.
 
ukisha jiunga na maccm lazima kaugonjwa ka kudanganya wananchi ukapate, muongo nae kawa mzee wa porojo
 
Ndugu wanajf nimekuwa nikifuatulia kwa karibu sana jinsi waziri wa nishati prof. muhongo anapolidangaya taifa letu kuwa hakuna mgao wa umeme. Je anafanya hivyo kwa maslahi ya nani wakati nchi ipo gizani? Leo nimefuatilia na kugundua kuwa zaidi ya mikoa kumi haina umeme. Hivi huyu ni prof kweli au ni prof kama vile wale wanaojiita hivyo? Namuomba aache mara moja kulidanganya taifa maana ulimwengu wa sasa si kama wa miaka ya arobaini na saba aliyozaliwa yeye! Kama ataendelea na uongo wake wanajf tuitishe maandamano ya kudai umeme na pia kumtaka waziri muhongo achie ofisi ya umma maana bado hatujafikia kuongozwa na waziri muongo.

Hatuna serikali, rais muongo, pm muongo, mawaziri waongo!
 
Ni kweli mgao umeanza kimyakimya hawajatangaza kama kuna mgao hapa ndiyo uone namna taaluma ilivyoingiliwa na siasa.

Kwanini Tanesco wanashindwa kutoa taarifa kwamba kuna mgao wa umeme? Niko Arusha kwa kama wiki sasa kila siku jioni saa kumi na mbili na nusu umeme unakatika unarudi saa nne na nusu au saa tano usiku ila usiku wa kuamkia leo umenyoosha giza mpaka asubuhi. Kwanini hawasemi? Au CCM itakosa kura kutoka kwa wadanganyika
 
Huku geita hii ni wiki sasa unakatika asubuhi na kurudi jioni....ukirudi unakuwa hauki stable....
Nadhani anazungumza ila hana ufahamu kuwa kile shirika linafanyaje kazi...
 
Poleni sana nduguzanguni.

Habari kama hizi zinaua moyo sana hata kama mtu unakusudia kurudi nyumbani.

Labda kama una mpango wa kupigana vita juu kabisa zinaweza kukutia moto kwamba utarudi kuzikabili.

Otherwise frustrations tu.
ukirudi tz utakuwa chizi,endelea kuenjoy ma wallmat,ma kfc,ma super bowl ma shopping malls,ma nba, ma mtv skyscraper na makila kitu
 
Back
Top Bottom