Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada awasili nchini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,859
4,673
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 19 – 23 Julai, 2023.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Sajjan alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo.

Akiwa nchini, Mhe. Sajjan pamoja na ujumbe wake anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali na kujadiliana nao masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Canada.

Aidha, Waziri Sajjan anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Afya pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Canada.

IMG_20230719_190735_739.jpg

IMG_20230719_190735_511.jpg
 
Canada yatoa msaada wa $25 millioni kusaidia sekta ya elimuIli Tanzania ifanye mapinduzi shule za sekondari kuwa na mifumo miwili mfumo wa masomo ya jumla na ule unaokazia masomo ya ufundi kwa vitendo na pia kusaidia watoto wa kike wenye changamoto shuleni kama mimba za utotoni amesema Waziri ushirikiano wa kimataifa na maendeleo wa Canada mheshimiwa Harjit Singh Sajjan mjini Dodoma Tanzania.
  • Tanzania is one of the largest recipients of Canada's international assistance ($127M in 2021-22). Canada has contributed $3.54 billion in development assistance to Tanzania since its independence.
  • Canada is among the largest bilateral donors for Tanzania in the health sector, providing significant support in health system strengthening, as well as SRHR.
Source : Minister Sajjan to travel to United Kingdom, Rwanda and Tanzania - Canada.ca
 
Back
Top Bottom