Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Kiongozi anapoteuliwa na Mheshimiwa Rais huwa anatakiwa kutekeleza majukumuu yake kikamilifu na kwa mafanikio lakini kwa hapa Tanzania Waziri wetu wa fedha ameonyesha ameshindwa Wizara hiyo kwa sababu hali ya uchumi wa nchi unavyokwenda.
Hivi majuzi Waziri alitangaza kuwa zaidi ya maduka 3000 yameacha kufanya biashara sehemu mbalimbali nchini kwa jinsi ya hali ya uchumi ilivyo kwa sasa. Je yeye kama Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo ameshindwa kujua tatizo la wafanyabiashara hao na amechukua tahadhari gani wafanyabiashara wengine wasifunge biashara zao?
Mpangilio wa ukusanyaji kodi kutoka kwa wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje si mzuri serikali iwekee bei elekezi kwa kila bidhaa inayoingizwa nchini badala ya kumtoza mtu kodi kiasi ambacho kinazidi mtaji wake. Wakati wa bunge lililopita baadhi ya wabunge walimtupia lawama Waziri husika lakini naona hakuna mabadiliko.
Mheshimiwa Rais Magufuli kazi ulioifanya mwaka mmoja wa kupambana na ufisadi na matumizi mazuri ya fedha za serikali ni nzuri sana kiasi ambacho watanzania wengi wamekubaliana na wewe cha muhimu hili suala la uchumi kidogo inaleta picha mbaya, Mhe. Rais tupia jicho wizara hii kabla mambo yasizidi kuwa mabaya. Nashangaa sana kwa Waziri kushindwa hata kushawishi mabenki ya nje na wafadhili kutupa msaada wakati huu wa matatizo ya kiuchumi.