KMKM Waziri wa Elimu Zanzibar azindua mradi wa ujenzi wa ofisi ya kikosi cha KMKM

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema Mradi wa Ofisi Katika kikosi Cha KMKM Wete utasaidia katika kuimarisha ulinzi na usalama katika Eneo Hilo.

Mhe. Lela ameyasema hayo mara baada ya kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Kikosi Cha KMKM iliyopo Uzunguni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Kwa Niaba ya Waziri wa Uchukuzi wa SMT Mhe. Makame Mnyaa Mbarawa katika Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mhe. Lela amesema kutokana na Ofisi hiyo Serikali inamatumaini Makubwa kwamba Wananchi wa Wete na Maeneo jirani watashirikiana kikamilifu na Maafisa na Wapiganaji katika kutoa taarifa za magendo na uharibifu wa mazingira ya bahari.

Aidha amesema kukamilika kwa miradi mbali mbali ya Ujenzi wa Ofisi za KMKM Kaskazini Pemba Serikali inamatumaini Makubwa kwamba Wananchi watashuhudia mabadiliko makubwa ya kiutendaji wa kikosi Cha KMKM Pemba.

Aidha amesema kutokana na haja ya kuwarekebisha tabia wale wote waliotiwa hatiani ni muhimu kutilia maanani wazo la Muasisi wa Mapinduzi la kutoa Mafunzo mbali mbali kupitia Chuo Cha Mafunzo.

Amesisitiza kwamba Falsafa hiyo ya Chuo Cha Mafunzo ndio inayotumika katika Mataifa mbali mbali kwalengo la kuwarejesha wahalifu Wakiwa raia wema.

Amesema kufanya hivyo mbali na kusaidia kuwajengea uwezo wahalifu lakini pia nikuyaenzi Maono ya Muasisi wa Mapinduzi Hayati Mzee Abeid Amani Karume.

Aidha Mhe. Lela ametoa wito Maalumu kwa Makamanda, Maafisa na Wapiganaji wa Vikosi vya KMKM, KZU na Chuo Cha Mafunzo kuendelea kutanguliza Maslahi ya Umma katika Utekelezaji wa majukumu yao.

Imetolewa na Kitengo Cha Habari na Mawasiliano (WEMA)
02/01/2024


FB_IMG_1704292274359.jpg
FB_IMG_1704292270169.jpg
 
Chadema siwani nawaona ccm tu. Akina Maria Sarungi wapo twitter huko wanaisifia Isreal inavyowaua watoto wa Palestina. Wanaharakati watz wengi wao wa dini
 
Hv katiba ya Jamuhuri inaruhu inchi moja ya TZ kuwa na vikosi ndani yakevya ulinzi.?
Kwa mnaofahamu mtueleweshe.
 
Back
Top Bottom