Mapambano Yetu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 1,133
- 2,128
Mh. Waziri wa Tamisemi ulitoa siku 30 kwa maafisa elimu ambao kimsingi waliwahamisha walimu kinyume na taratibu kuwalipa stahiki zao ndani ya siku 30. Naomba kukujulisha kuwa tamko lako waliliacha pale pale kwenye kikao. Ninamifano hai na evidence kuhusu hili suala. Kwa Kuanzia Naomba umwulize afisa elimu mkoa wa Morogoro akwambie ana malalamishi mangapi ya walimu ambao uhamisho wao haukufuata vigezo. Uhamisho ambao kiini chake ni Wakuu wa shule kutopenda kuulizwa au kuhojiwa kuhusu mapato na matumizi ya fedha za shule, Wakuu kuendesha shule kwa mazoea (yeye anakuwa mhasibu, storekeeper, mtaaluma, manunuzi, nidhamu nk), Wakuu ambao kimsingi wanajifanya miungu watu shuleni.
Mh. Waziri tangu lini kurekebisha IKAMA kukamtoa mwalimu sehemu ambayo ilikuwa na walimu 2 wa somo hilo (akiwa na vipindi zaidi ya 35 kwa week) akapelekwa sehemu yenye walimu 4 wa somo husika na kupewa vipindi kati ya 12 - 18 kwa week? Nina ushahidi wa kilichotokea Morogoro kama Afisa Elimu atakana nitaweka hadharani ushahidi wote wa kilichotokea.
Mh! Waziri sawa walimu wamehamishwa basi walipwe stahiki zao zote ili wakapige kazi mahali walipopangiwa, kulazimisha waende bila kuwalipa stahiki zao ni kosa kisheria. Kuna maafisa elimu wanawalazimisha walimu waende kwenye vituo vyao vipya ilhali fedha za uhamisho hawajawapa. Huu sio uungwana.
Naomba nihamie kwa waziri wa Elimu.
Mh! Waziri hivi unajua kuwa baadhi ya shule za Morogoro zinaongozwa na wanasiasa? Hawa sio Wakuu wa shule wala sio waalimu lakini wanachokiongea wao ndo kinafanyiwa kazi hata kama ni cha kubomoa. Shule inaweka mipango ya kujenga hostel, au hata madarasa kwa ajili ya kidato cha tano na sita lakini ndani ya miaka 4 - 5 unajengwa msingi tu. Akijitokeza mfadhili figisu figisu mpaka anaghairi. Wanasiasa wanataka wafadhili wawape wao fedha ili wakasimamie hiyo miradi na jamii ifumbwe macho (vijijini) bila kujua yanayoendelea.
Mh! Waziri majengo Mengi ya shule yamejengwa chini ya viwango. Utakuta jengo limejengwa mwaka 1 linanyufa utadhani ni la miaka 50 iliyopita. Wakuu wa shule, watendaji kata wanayajua haya na ten % walishiriki kuigawana (kama sio 60%). Miaka kumi ijayo serikali lazima iingie hasara ya kujenga upya madarasa maana kilichokuwa kikifanywa na hawa watendaji ni danganya toto tu. Ela ilipigwa to the maximum level.
Mawazo yangu
1. Walio hamishwa walipwe
2. Maafisa Elimu waache kuegemea upande wa Wakuu wa shule tu.
3. Hata Wakuu wa shule waache kuongoza kwa mazoea
4. Serikali iajiri walimu hasa wa sayansi maana hali ni mbaya sana na kwa uhamisho wa visasi uliopita, hali ndo imevurugika kabisa.
5. Majengo na thamani yake yahakikiwe upya. Tena hili lifanywe kwa umakini wa hali ya juu sana maana hata wafanyakazi kwenye halmashauri walihusika kupiga ela.