Waziri wa Elimu atinga St. Joseph university

dekitambi

JF-Expert Member
Oct 5, 2015
663
761
Chuo Kikuu cha Mt. Joseph kimechukua vichwa vya habari hivi karibuni baada ya kutokea kwa migomo kwenye vyuo vishiriki vya chuo hicho na baadhi kufutiwa vibali vilivyoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mt Joseph ambavyo ni chuo kikuu kishiriki cha sayansi ya kilimo na Teknolojia ‘SJUCAST’ na chuo kikuu kishiriki cha teknolojia ya Habari Mawasiliano ‘SJUIT’.

Chuo cha Mt Joseph nao waligoma kuanzia mwanzoni mwa juma hili wakiwa na madai mbalimnbali ikiwemo kufundishwa mtaala ambao haupo nchini pamoja na wakufunzi wasio na sifa.

Leo March 9 Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amefika chuoni hapo na kutoa maelezo ikiwa ni juhudi za kutatua mzozo huo na ameyazungumza haya kwa wanafunzi…

’Baada ya kuona changamoto nyingi kuwa ni za kiutawala, kwa hiyo mmalizie mitihani yenu, baada ya mitihani ni wiki mbili, kwa hiyo chuo kitakuwa kimefungwa, muda huo Chuo kirekebishe dosari ndogondogo hizi za kwenye maabara, vitu ambavyo havijafungwa na vimekwisha kufika vifungwe na kikubwa zaidi ni suala la kiutawala kwa wale ambao hawana sifa Utawala urekebishe‘:-Joyce Ndalichako

Pia Waziri Ndalichako amegusia madai ya ada kubwa chuoni hapo na ameyazungumza haya

‘Suala la ada ni suala ambalo linatakiwa liangaliwe kwa ujumla wake kwa vyuo vyote kwa sababu mwanafunzi anapojiunga na chuo anajua ada ni kiasi kadhaa, kwa hiyo kwa kusema kwamba itapungua hilo ni suala la makubaliano, na kwa kuzingatia kwamba TCU inaangalia namna ya kuweka ada elekezi kwa vyuo vyote kwa hiyo sasa hivi wanafunzi watatakiwa kulipa ada kama makubaliano yalivyo wakati makubaliano yale yanaendelea’:– Joyce Ndalichako

Chanzo: Millard Ayo
 
ukitaka info zaidi tembelea Millard ayo ... nimeanza kuikubali jammii forum juzi humu nimeona Uzi ukieleza st Joseph ni jipu majibu tumeanza kuyaona
 
Jamii Forum ina mchango mkubwa kwa Prof. Ndalichako kuukwaa uwaziri
 
Back
Top Bottom