Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amepokea mfano wa hundi yenye thamani Sh. 222.2. milioni kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka Taasisi ya BAPS CHARITIES,Subhash Patel kwa ajili ya kusaidia watoto 101 wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, iliyopo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) ,jijini Dar es Salaam.
Aidhampaka watakapofikia watoto wawili ambao wanasuburi kufanyiwa upasuaji wa moyo ,aliowahidi kuwasomesha mpaka watakapofikia mara baada ya kupokea msaada huo.Watoto hao ni Beatrice Daffi umri wa miaka 13 ambaye amesema anataka kuwa muuguzi ili asaidie wagonjwa wengine na kulia ni Zahara Selemani umri wa miaka 10.
Akipokea msaada huo Waziri huyo aliushukuri ujumbe huo kwa msaada walioutoa kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao, ili waweze kuendelea na masomo na kukua kama watoto wengine wenye afya bora.
“ Ni jambo zuri ninaamini kupitia kwenu taasisi binafsi na za Serikali, za dini ,nyingine za kijamii zitaguswa. Kuna watoto 500 kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar wanaosubiri kufanyiwa upasuaji kwenye taasisi hii. Hivyo kupitia msaada huu bado kuna watoto 399 wanohitaji kusaidiwa.
“Ninatoa wito watu mbalimbali wajiunge mkono jitihada hizi.Pia ninapenda kumpongeza Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne kwa uwekezaji huu ambao umesaidia kupunguza kwa zaidi ya asilimia 55 ya wagonjwa wanapata rufaa ya kutibiwa nje ya nchi.
Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza jitihada hizi kwa kujenga uwezo wa kutoa huduma, bali changamoto iliyopo ni kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kutosha,” alisema Waziri Ummy huku akisisitiza watafute na watoto wengine kutoka sehemu za vijijini mfano Rukwa na Katavi.
Aliongeza kuwa kinachotakiwa nio kumwomba mwenyezi Mungu ili upasuaji uende salama.
Alisema watawaalika baadhi ya watalamu kutoka nje ya nchi ili waweze kusaidiana na wataalamu waliopo nchini kufanya upasuaji huo.
Waziri Ummy alifafanua kwamba ili kuweza kuepuka magonjwa ya moyo kwa watoto ni muhimu kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, kupata chanjo ya Rubela kila mwezi.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Naizi Majani alisema akiwa mamamjamzito na watoto wote wapata chanjo zote inasaidia kupunguza kwa asilimia 10 magonjwa ya moyo.
Kwa upande wake, Patel alisema msaada huo ndio mwanzo wataendelea kutoa mingine.
“ Tunawasaidia watoto hawa tunaamini watapata maisha mapya na watakuwa Watanzania bora na waaminifu,” alisema Patel.
Msaada huo utawezesha watoto kumi kufanyiwa upasuaji kila mwezi.caption za picha ziko chini.