Waziri wa afya Ummy Mwalimu awatoa wasiwasi Wazee

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
879
969
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bi Ummy Mwalimu amewatoa wasiwasi wazee kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya

Akizungumza na baraza la wazee wa Dar es salaam Bi. Mwalim amesema serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee ikiwemo kuanzisha mfuko wa wazee ambao utawasaidia kupata mikopo ili kujikwamua kimaisha na pia kutoa huduma za afya bure kwenye hospitali za serikali .

Bi Mwalim amesema wizara yake itapeleka sera ya sheria ya wazee bungeni ili iweze kujadiliwa sera ambayo itasaidia sana kutatua changamoto mbalimbali za zinazowakabili wazee.

Kwa upande wa wao baadhi ya wazee wametoa mapendekezo yao kwa waziri ambapo wameombwa kuwepo na ushirikishwaji wa karibu wa wazee pamoja na uwakilishi katika sekta mbalimbali
 
Nao hawajitambui hawa, hakuna siku madai yao yamepatiwa ufumbuzi, wakistaafu hata pensheni ambayo ni halali yao kupata ni zengwe, matibabu ya bure ni tatizo, lakini wakiitwa kwenda kumsikiliza rais, wanafurika mpaka ukumbi hauwatoshi, wangeweka mgomo wakae makwao rais akute viti vitupu, ndio wangekumbukwa na ahadi kutekelezwa, wanadanganywa kama watoto wadogo, daily!
 
Back
Top Bottom