Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Katika kuelekea kusheherekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mh.Ummy Mwalimu ,leo kwenye taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo hospitali ya Taifa Muhimbili,amejitolea kuwasomesha watoto wawili wa kike Zahara Selemani kutoka Meru na Beatrice Daffi kutoka Karatu,waliolazwa hospitalini hapo kusubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.Wakati akipokea msaada wa shilingi milioni 222,200,000 kutoka taasisi ya Baps Charities.Kaulimbiu ya maadhimisho mwaka huu inasema "50-50 ifikapo 2030;Tuongeze Jitihada"