Ile changamoto ya machinga kuziba barabara naona imeanza kurudi upya. Leo nimepita mitaa ya Liberty Mwanza hapafai tena kumerudi kama zamani.
Wananchi wanadai kua mgambo wa jiji ni kama wameingia woga na wengine wana mgomo baridi baada ya lile sakata la juzi na namna waziri TAMISEMI alivyolifanyia kazi.
Ni kweli wale mgambo walikosea na walipaswa kuwajibishwa... lakini kutilia mashaka kama RC na DC wanatosha kwenye nafasi zao nadhani waziri alienda mbali kidogo
Kwa namna ambavyo hawa ndugu zetu wamachinga wanavyorudi kwa kasi serikali ilipoteza tu rasilimali zake kupambana nao kipindi kile.
Mkuu ukipita buhongwa,mpaka kero asee,hakuna mtu anakataa watu kutafta ugali,Sasa watu wako barabarani kabisa,hata gari likikosea njia,asilimia kubwa ya watu watakuwa wameumia.kialisia jiji la mwanza limewashindwa machinga