Waziri Tamisemi tumbua majipu wakurugenzi wa manispaa za jiji la Mwanza, Hali ya barabara inatisha

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,908
2,773
Barabara nyingi za jiji la Mwanza zina hali mbaya, hazipitiki na zinachangia kwa kiasi kikubwa kualibu magari ya watumiaji wa barabara hizi, ni aibu kwa manispaa za jiji la Mwanza kushindwa kuwa na mkakati wa kujenga barabara za muhimu kwa njia ya rami mpaka kutegemea misaada kutoka serikali kuu, tunaomba waziri wa tamisemi awatumbue majipu kama wameshindwa kusimamia ubora wa miundombinu katika jiji la Mwanza.
 
Wakurugenzi wengi wa halmashauri ni majipu..!! Wengi pia uwezo wao mdogo, maana waliishi kwa kubebana na kujuana kwenye utawala uliopita.
 
Nafikiri tatizo si kujenga barabara. Barabara za jiji la Mwanza zimejengwa miaka michache iliyopita. Tatizo kubwa ni kutokuwa na utaratibu wa kukagua na kufanya marekebisho (Preventive maintenance) ili kuhakikisha barabara zinadumu. Hili si tatizo la Mwanza tu ni tatizo la nchi nzima. Hakuna kitu kinachodumu milele hata kama kingekuwa imara namna gani. Hivyo kutokuwa na utaratibu wa kukagua na kufanya marekebisho/matengenezo ya mara kwa mara kunachangia uharibifu mkubwa zaidi. Kwa nini miji na majiji yasiwe na vitengo vya ujenzi vyenye mainjinia wazawa ambao wanaweza kufanya kazi hiyo??
 
Lipeni pia kodi halali kwa wakati zifanye kazi za kujenga barabara! Tusiwalaumu tu viongozi!
 
Back
Top Bottom