Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene amesema kuwa kwa sasa Serikali itazingatia uzoefu wa kufundisha shule za Msingi ktk kutoa vyeo vya Uafisa Elimu kwani walimu wenye uzoefu huo wanaijua Elimu na changamoto zake.
Ameyasema haya katika ukumbi wa Kambarage ktk Jengo la Hazina mjini Dodoma katika Uzinduzi wa Ripoti ya [HASHTAG]#KiuFunza[/HASHTAG] ambao ni utafiti uliofanywa na Twaweza ambao ulihusisha kutoa Motisha ya Fedha kwa walimu wanaofundisha vema katika masomo ya Hesabu, Kiswahili na Kiingereza.
Utafiti huo umeonesha matokeo chanya katika wilaya zilizochaguliwa zikiwemo Ubungo na Mbinga ambazo zimetoa shule zilizofanya vema. Katika shule ambazo bahshishi kwa walimu ilitolewa, matokeo yalikuwa mazuri ambapo ufaulu wa Kiswahili na Hesabu uliongezeka hadi kwa asilimia 20.
Walimu katika shule hizi wamepewa zawadi za fedha kulingana na idadi ya wanafunzi waliofaulisha. Mwalimu Neema Maro wa Shule ya Msingi Milenia ya Tatu amepatiwa kiasi cha zaidi ya Milioni 3 na Laki 6 kwa kufaulisha vizuri ambapo kwa somo la Kiingereza amefaulisha takribani mara 8 ya wastani wa ufaulu kitaifa.
Waziri Simbachawene pia aliwapigia debe walimu waliofanya vizuri kwa Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI na kumuomba awakumbuke kwa vyeo kwani haiwezekani mtu afanye vizuri halafu abaki palepale.