Waziri Simba aendeleza usanii katika utendaji wa Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Simba aendeleza usanii katika utendaji wa Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 29, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,135
  Trophy Points: 280
  Waziri Simba: Tupo makini, tutawashughulikia
  Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 29th January 2010

  Habari Leo

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, amesema, si kweli kuwa Serikali inachelewa kutoa uamuzi au haitoi uamuzi sahihi kuhusu vitendo viovu ukiwemo ubadhirifu wa mali ya umma na mikataba mibovu.

  Waziri Simba pia amelieleza Bunge kuwa, si kweli kuwa Serikali haikemei vitendo viovu ukiwemo ukiukwaji wa maadili.

  Simba amewaeleza wabunge kuwa, Serikali ipo makini kuhakikisha kuwa uamuzi wowote inaoutoa uwe sahihi na wakati mwingine inabidi ifanye utafiti au uchunguzi wa kina kabla ya kutoa uamuzi.

  “Maamuzi ya Serikali hayawezi kufanywa bila kufanyiwa kazi na bila kuzingatia taarifa zilizopo mikononi mwa Serikali...lengo la kufanya hivyo si kuchelewesha uamuzi bali ni kuhakikisha kuwa uamuzi unaotolewa na Serikali unakuwa ni sahihi, unaozingatia sheria, haki na maslahi ya taifa” amesema Waziri Simba wakati anajibu swali la Mbunge wa Kalenga, Stephen Galinoma.

  Mbunge huyo amedai kuwa, majibu ya Serikali ni ya nadharia zaidi kuliko vitendo, Waziri Simba amekanusha.

  Galinoma pia alimuuliza Waziri Simba ni kwa nini Serikali haikemei maovu na ikasikilizwa kama zamani na kwamba, Serikali haioni kwamba, mambo hayo yanaashiria kuporomoka kwa utawala bora katika taifa letu.

  “Katika miezi hii ya karibuni taifa limeshuhudia mambo mengi mabaya katika jamii, kwa mfano mikataba mibovu, wizi, na ubadhirifu wa kiwango cha hatari, migomo mbalimbali na matukio ya hapa na pale ya wananchi kujichukulia sheria mkononi” amedai Mbunge huyo.

  Simba amelieleza Bunge kuwa, matukio mengi ya wizi, ujambazi na uovu mwingine haviashirii kuporomoka kwa utawala bora nchini.

  Waziri Simba pia amewaeleza wabunge kuwa, uchu, tamaa, na pupa ya utajiri wa haraka vimesababisha ongezeko la uhalifu nchini. Amesema, uovu huo ikiwemo migomo ni makosa ya jinai yanayofanywa na watu wachache wanaokiuka misingi ya maadili na sheria.

  “Huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine wowote. Serikali itaendelea kupambana nao kwa nguvu zake zote” amesema Waziri Simba.

  Amesema, Utandawazi umesababisha ongezeko la uhalifu nchini kwa kuwa watu wanaiga tabia na vitendo vya watu wa mataifa mengine.

  “Kuhusu Mikataba mibovu, na ubadhirifu wa mali ya umma, Serikali na vyombo vyake vinaendelea kuchunguza, kufuatili na kuchukua hatua zinazostahili kwa kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuhusika kwa njia moja au nyingine” amesema kiongozi huyo wa Serikali.


   
 2. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Mimi bwana huyu mama akisema siku hizi, huwa sitoi comments. JK alipokwenda Same kuwapa pole watu kwa mafuriko, alisema; Anna Kilango unaisema sana serikali yangu...!. Hiyo ni muda mfupi baada ya Sofia Simba kulipuka kuhusu Anna Kilango kwenye kamati ya Mwinyi kwamba Ana Kilango anapiga kelele kwa sababu kaukosa U-first lady na.....! Kauli ya JK ilikuwa mwangwi wa maneno ya Sofia Simba kwa kamati ya Mwinyi.

  Kwenye suala la kuongoza serikali, kama kuna issue tata yoyote, njia nzuri ya awali kuitatua ni kwa wahusika wakuu kujiuzu. Iwapo wahusika wakuu hawajiuzu, mbali ya kutochukuliwa sheria, inatia shaka sana sana. Hata kama hawahusiki moja kwa moja, kuachia ngazi ndiyo utawala bora Duniani kote. Mimi ningekuwa Galinoma, ningemwambia wazi Waziri kuwa: Lowasa, Karamagi, Msabaha, Mwakapugi, Manyika na mwenyekiti wa board ya Tanesco by then wajiulu instantly. Achilia mbali chenge na wenzake.

  lakini ndiyo siasa.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
   
 4. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
   
Loading...