Waziri Prof. Muhongo, TANESCO inahujumu wananchi kwa kushirikiana na mitandao ya Simu

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,772
7,141
Wana JF,

Kuna biashara chafu kati ya TANESCO na mitandao ya simu, watu wengi wanahangaika kupata huduma kuwasiliana na TANESCO ili waweze kuelelezea matatizo yao, wahudumu wa call centre no. 0768985100 , wahudumu hawa ubonyesha call waiting key na kuicha simu hewani bila kuijibu, utasubiri muda mrefu bila mafanikio huku mitandao ya simu wakiendelea kutafuna fedha, mwishowe unashutuka pesa imeisha, Tanesco haijawahi kuelezea kuwa ukipiga kwenye numba hii unaliwa pesa, nimeenda tanesco Tegeta tukakutana watu wengi wakilalamikia huduma hii inavyowapotezea muda pamoja na kuliwa pesa bila sababu. Hata ukipiga kwa namba za huduma (emergency) wanakuelekeza kwenye no. hii, inaonekana kuna kamchezo kwa kuwa hii call center inatumiwa mkoa mzima.

Tunakuomba Waziri uingilie kati hii call center iwe na matumizi sahihi au kutafutwe njia nyingine ya kuwasiliana na wateja bila kupoteza muda na fedha.

Inashangaza sana huduma ya chengi key ili kuingizwa tarrif mpya inachukua siku tatu wakati ni kitendo cha dakika kadhaa
 
Back
Top Bottom