Waziri Nchemba kula sahani moja na wauza madawa ya kulevya

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,786
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato.

Waziri Nchemba ametoa agizo hilo mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi.

Screenshot from 2016-06-13 14:46:39.png

Mtanzania Jackie Cliff
 
Kweli atawaweza?maana nao wamejipanga kwelikweli kama brother ****** tu kawashinda itakuwa hao?labda kama kaokoka kwahiyo roho Mtakatifu atamfunika kwa damp ya bwana Yesu Kristo
 
Mwache aonje sumu kwa kuilamba ,sisi tutasalia kuwa watazamaji tu...
 
Back
Top Bottom