Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,354
Polisi nane wameuawa na mmoja kujeruhiwa huko Bungu mkoani Pwani walipokuwa wakirudi kambini baada ya kubadilishana lindo katika kizuizi.
Binafsi ninatoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wote.
Nina matumaini kwamba uchunguzi wa kina utafanyika ili kubaini wahusika wa tukio hili na kujaribu kuzuia matukio kama haya.
Askari hawa wameuawa usiku wa mkesha wa siku ya Ijumaa kuu siku muhimu ya mwanadamu ambae ni mkristo kutafakari mateso alipata mwokozi Yesu Kristo miaka takriban 200 ilopita, mateso yaloanzia kwenye bustani ya Gesthemane.
Kuuawa kwa vijana hawa kunaendelea kuweka rekodi ya mauaji ya askari polisi ambao ndiyo walinzi wa Amani, na pia ndiyo wenye jukumu la kulinda mali na usalama wa raia.
Tayari jeshi la polisi lilikwishapoteza askari wake mwezi Julai mwaka 2015 huko Stakishari Ukonga ambako kituo cha polisi kilivamiwa na majambazi na askari 4 na raia watatu na kupora silaha kutoka katika ghala la kuhifadhia silaha.
Pia kulikuwa na tukio la benki ya CRDB tawi la Mbande kuelekea Chamazi kuvamiwa na majambazi na askari mmoja waliuawa na bunduki aina ya SMG ikachukuliwa.
Mwezi February mwaka 2013 majambazi walivamia eneo la Mchicha katika eneo la TAZARA na kumuua askari mmoja na kuwajeruhi vibaya askari wengine wawili
Tarehe 10 April mwaka huu, majambazi wawili walivamia maduka katika maeneo ya Sinza na Tegeta katika kujaribu kupora fedha.
Katika mapambano na polisi majambazi hayo yalishindwa kwa kupigwa risasi na kwenda kufia hospitali ya Muhimbili.
Mkuu wa mafunzo na operesheni CP Msato Marijani Massanzya leo akiongea na waandishi wa habari amedai kwamba matukio haya ya uvamizi, uporaji na mauaji ya askari polisi na viongozi wa serikali za mitaa mkoani Pwani kuwa si ya kigaidi bali ni ujambazi wa kawaida.
Pia amedai kwamba jeshi la polisi limeanzisha operesheni maalum kujaribu kuwabaini majambazi hawa au watu wanaojihusisha na aina hii ya mauaji ya polisi na uporaji silaha.
Kwanza ningependa kumkumbusha kamishna Massanzya kwamba mtindo huu wa mauaji ya askari wetu na uporaji wa silaha unaota mizizi kuanzia tukio la Stakishari hadi hili la sasa, hivyo kuzidi kujenga hoja kwamba mpaka sasa bado jeshi la polisi halijaweza kuja na mpango wa namna ya kukabiliana na mtindo huu wa ujambazi.
Mtindo huu wa uhalifu ni ule wa kupangwa kiufundi yaani "serious organised crime" ambapo kuna kikundi au kundi la raia wenzetu ambao wameamua kwa makusudi kuleta hofu ndani ya nchi hii kwa kuanza na kuua askari polisi.
Mara nyingi mipango ya wahalifu kama hawa hufanywa nje ya mji kama huko Kibiti mkoani Pwani, hivyo kuashiria wazi kabisa pasi na shaka kwamba tuna vikundi hatari vya uhalifu nchini Tanzania hususani mkoani Pwani.
Hali hii inaashiria kwamba kuna kasoro mahali Fulani na inashabihiana moja kwa moja na ukosefu wa mafunzo imara na mbinu za kujilinda kwa askari hawa wanapokuwa lindo, wanapobadilishana lindo na utaratibu mzima wa kusimamia malindo.
Ikiangalia kwa mfano tukio la Chang'mbe ambapo polisi mmoja aliuawa na wawili kujeruhiwa, majambazi yalikuwa kwenye gari muda wote wakiwasoma na kuwabaini makosa yao (polisi) na kisha kuwafanyia ambush na kuleta madhara.
Hii pia inaenda sambamba na mbinu za ulinzi katika vituo vyetu vya polisi ambapo mara nyingi utakuta polisi wanalala juu la meza kuu au "counter", hali ambayo ni tofauti na kituo cha kijeshi ambapo katika ile "gatehouse" yaani pale getini utaona mwanajeshi amesimama wima na ameshikilia bunduki yake akiwa tayari kwa lolote.
Polisi siyo wanajeshi lakini wanapaswa kuwa na mbinu za kujihami na kujilinda khasa katika suala la ulinzi wa vituo vyao, kambini na kwenye malindo kama vile kwenye mabenki na katika miundombinu ya serikali.
Lakini tukio hili la mauaji ya jana yanaleta masuali mengi kuhusu uendeshaji wa jeshi hili na wizara nzima ya mambo ya ndani.
Nakumbuka IGP Mangu na msaidizi wake Abdulahman Kaniki walipoteuliwa na raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete mwaka 2014, waliapa kuhakikisha kwamba Imani ya raia kwa jeshi la polisi inaimarishwa.
Kukiwa na Imani kwa jeshi la polisi kutoka kwa raia kunaleta Amani na ushirikiano ambapo raia wanaweza kulisaidia jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za kiintelijensia ambazo zinaweza kuzuia na kukomesha ujambazi kama huu wa Kibiti.
Nina imani kabisa kwamba wananchi wa mkoa wa Pwani wanawafahamu wahalifu hawa na labda kutokana na matatizo ya imani na ushirikiano kuwa haba basi majambazi wanakuwa wamepata pa kujificha.
Kabla ya kuteuliwa kuwa IGP Ernest Mangu alikuwa mkurugenzi wa idara ya Intelijensia katika jeshi la polisi, hivyo kazi yake kubwa ilikuwa ni kujenga Imani ya wananchi kwa kuwekeza katika mawasiliano mazuri na ushirikiano ambapo hadi leo tusingekuwa tunasikia mauaji ya polisi.
Ninaamini kabisa uwezo na elimu ya IGP Ernest Mangu katika kuongoza jeshi hilo lakini inaonekana kwa sasa ameelemewa na anapaswa kujitathmini kuhusu nafasi yake.
Inawezekana ni ujuzi, au vitendea kazi, au uhaba wa fedha yaani bajeti ndogo lakini ni wakati sasa wa jeshi letu kuongozwa kisasa na pia kutosita kuomba msaada kutoka katika mataifa yenye ujuzi katika masuala ya uendeshaji wa jeshi la polisi.
Suala la bajeti ndogo au muundo wa jeshi hili linapaswa kuangaliwa zaidi na waziri husika mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambae nae tangu kuteuliwa kushika nafasi hiyo amekuwa kimya sana.
Lakini kama mheshimiwa Mwigulu Nchemba na IGP Mangu wanaona kazi ni ngumu basi litakuwa ni jambo la kheri na busara ikiwa watapisha na nafasi zao kushikwa na watu wengine wenye uthubutu.
Tunahitaji jeshi la Polisi imara ambalo halijihusishi la vitendo vya unyanyasaji wa raia bali lenye kuwalinda na kuhakikisha usalama wao na mali zao.
Lakini pia tunahitaji jeshi la polisi lenye vijana wakakamavu, weledi, wenye kufahamu majukumu yao na wenye kuheshimu na kuifuata sheria.
Pia tunahitaji waziri wa mambo ya ndani ambae ana mipango ya kulijenga jeshi hilo liwe la kisasa.
Bila kutaka kuonyesha wazi kwamba naingilia kazi ya waziri lakini nina Imani kabisa kwamba hadi sasa hakuna kanda maalum au "zones" ambazo zinajulikana kwamba zinalea majambazi .
Pia inaonekana wazi kwamba hakuna kanzi data au "database" ya wahalifu wote jambo ambalo linaweza kusaidia kuwadhibiti mienendo yao.
Litakuwa jambo la faida sana kama ukaundwa mfumo wa waleta habari au "infomers" ambao huweza kupatikana tu ikiwa kuna ushirikiano kati ya jeshi la polisi na raia.
Pamoja na kwamba kuna namba maalum ya "crimestoppers" lakini haukonyeshi kwamba kuna data zinazoonyesha kwamba taarifa za kijasusi zinarekodiwa na namba hiyo kiasi cha kuacha hiyo namba sasa hata kutumiwa na baadhi watu ambao kamanda Sirro amewahi kudai huwa wanampigia hadi usiku wa manane.
Kwanini Kamanda Sirro apigiwe simu yake yeye mweneywe badala ya simu zote kuelekezwa kule "call centre"?
Kituo cha Crimestoppers kipo kwa ajili ya kusaidia kupata taarifa za kihalifu.
Ni wakati sasa wa waziri Mwigulu Nchemba na IGP Ernest Mangu kujitafakari.