Waziri Mwakyembe: Hakuna sheria inayokataa mikutano ya kisiasa baada ya Uchaguzi

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,400
24,982
Dkt. Mwakyembe ametoa rai hiyo leo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Amesema, Tanzania haina sheria wala kanuni zinazo wadhibiti na kuwasimamia wanasiasa kuhusu namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao jambo ambalo limekuwa likileta mvutano akitolea mfano zuio la kuendesha shuguli za kisiasa nchini hadi uchaguzi wa mwaka 2020 ambao unalalamikiwa na vyama vya upinzani.

20170214204045.jpeg


Chanzo: EATV
 
Kwahiyo mitano ya vyama itaanza mini hata cc huku kwenye nchi hakuna raga bila mikutano, tumesherehekea miaka 40 kavu kavu, vipi...???
 
Hapo amekiri ukweli kwakuwa kakutana na wanasheria hivyo imebidi atumie akili, lakini angekuwa nje ya hapo angeongea kwa kutumia tumbo. Alijua kabisa akileta hadithi za kutetea tumbo atapewa kubwa yake hivyo akawa hana ujanja kwenye mazingira hayo. Hao ndio wanasheria wetu tulionao ambao wao kuliko watete ukweli kulingana na taaluma zao bora atetee tumbo lake hata kama litadhalilisha taaluma yake. Kweli njaa mwanaharamu wallah mpaka elimu inageuka bure kabisa.
 
Leo Mh.Waziri Mwakyembe amekuwa Na mkutano Na wanachuo Kikuu cha DSM Shule ya Sheria.Akijibu swali Kutoka Mwanachuo Juu ya uwepo wa Sheria inayokataza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi.Akijibu swali hilo Mh.Waziri Mwakyembe amekiri kutokuwepo Kwa Sheria wala kanuni yoyote.Kutokana Na majibu hayo je Mh.Mwakyembe kwanini hukumshauri Mh.Rais juu ya kutokuwepo Kwa Sheria hiyo? Je zuio hilo sio halali?
 
Back
Top Bottom