Waziri Mwakyembe amtembelea Wastara, ampa milioni moja

Waziri Mwakyembe amtembelea Wastara, ampa milioni moja

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Waziri Mwakyembe amtembelea Wastara, ampa Mill. Moja.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe jana Januari 20, 2018 amemtembelea na kumjulia hali msanii wa filamu Wastara nyumbani kwake Tabata Sanene, Dar es Salaam.

Wastara kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mguu na yupo kwenye maandalizi ya safari kwenda India kwa matibabu zaidi.

Waziri Mwakyembe akiambatana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu na Katibu Mtendaji wa BASATA alimtakia kheri Wastara na kumkabidhi mchango wa Shs. 1,000,000/= (milioni moja).

Aidha, Mwakyembe aliwasihi wasanii na Watanzania kwa ujumla kumchangia Wastara kwa hali na mali ili aweze kupata fedha za kumwezesha kwenda India kwa matibabu zaidi.

Chanzo: Clouds Radio


26907102_1709655719077839_4243644683876960340_n.jpg
 
hivi huyo wastara hanaga chama cha waigizaji wenzie wamchangie ??
 
Huyu dada mbona kuna wakat alijinasibu kuwa ana biashara kadhaaa eg. Car Wash, Boutique n.k, pia ile hela ya kampeni 2015 hakusevu?
 
alianza kupata maumivu akiwa kwenye kampeni za ccm,nadhani alikuwa anakata mauno sana na kurukaruka,hao hao ccm wamsaidie,steve nyerere ndiye aliwakusanya,
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] .mkuu utakua na ka video kokote ili nione jinsi alivyokua akimwaga miuno
 
Kamanda niaje!Huyu anachangiwaga sana.........ndy kusaidiana kupi lkn Huyu ulemavu wakeanautumia kama mtaji...
Muamala ukishajaa soon ataanza kuvimba

Ova
Hilo liko wazi ..mimi nlijiuliza gharama ya kutibu mguu 37m mana ndio kasema...appolo cancer kuchoma mionzi mpka unarudi humalizi 10000$$.
Sasa yeye huu mguu plus hotel na ndege hamalizi 15m ila anataka apite dubai kufanya manunuzi na kuuza sura.....hata alipoenda mara ya mwisho alipita dubai kuuza sura na shopping.....mimi nlisikia anaduka la nguo na carwash tabata kua yuko njema
 
Hilo liko wazi ..mimi nlijiuliza gharama ya kutibu mguu 37m mana ndio kasema...appolo cancer kuchoma mionzi mpka irudi humalizi 10000$$.
Sasa yeye huu mguu plus hotel na ndege hamalizi 15m ila anataka apite dubai kufanya manunuzi na kuuza sura.....hata alipoenda mara ya mwisho alipita dubai kuuza sura na shopping.....mimi nlisikia anaduka la nguo na carwash tabata kua yuko njema
Hakuna watu wajinga kama hao wasanii wanaishi kwa maigizo tu
Wanaishi maisha ya kuwaiga Wakina Kardashian tu

Ova
 
Back
Top Bottom