Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Waziri Mwakyembe juzi amedanganya bungeni kuwa mfumo wa serikali wetu tunaotumia ni (Parliamentary system of Government) yaani Serikali inayotokana na Bunge, maskini Mbunge wangu wa Geita Joseph Msukuma na Mwenzake Lusinde kwa vile hawajui kitu wakashangilia kweli kweli.
Na akaendelea kuwashika masikio kuwa wanachokifanya mawaziri wanatumia mfumo wa (Collective ministerial Responsibility) yaani Mawaziri kuwajibika kwa pamoja kwa serikali ndio maana haikosoi serikali, nikasikia makofi pwaa! pwaa! pwaa! Akaamua kutumia katiba Ibara ya 52 ili wakina Goodluck Malinga kombani waamini Dr wa Sheria hadanganyi ili ahalalishe uogo wake wa kutetea tumbo lake.
Ngoja niwasaidie waliokuwa wanampigia makofi ili wajue alikuwa anawadanganya na siku nyingine wasimuamini tena, hivi ni kweli kukaa kimya uvamizi wa clouds tv na Nape kutolewa Bastola ndio Collective Ministerial Responsibility sio kweli huu ni uoga wao wa kumuogopa Makonda maana wanaweza kuhatarisha ulaji wao mfano mzuri kilichotokea kwa Nape.
Ndugu yangu Joseph Msukuma (Geita), Njaru Salanga (Itilima), Lusinde pamoja na wabunge wengi wa ccm mliopiga makofi, kwa sababu ya kutokujua, collective Ministerial Responsibility hii ni aina ya serikali inayotumia mfumo wa uingereza yaani Westminister model.
Kutokana na mfumo huu wa uwajibikaji wa pamoja wa Mawaziri, wajumbe wa Baraza la mawaziri ni lazima waisapoti serikali hadharani kwa maamuzi ya serikali ambayo yameadhimiwa kwenye baraza la mawaziri hata japo kuwa waziri mmoja hajalidhika nayo, Ila ni kwa maslahi ya taifa.
Swali langu hivi uvamizi wa Clouds Tv na nape kutolewa Bunduki yalikuwa ni maadhimio ya Baraza la mawaziri mpaka mawaziri wanakaa kimya, Je hayo matukio yalikuwa yana maslahi gani kwa taifa?,.
Baraza la mawaziri kuwajibika kwa pamoja ni tamaduni ya Parliamentary government (Serikali inayotokana na Bunge), katika aina ya serikali hii waziri mkuu anao wajibu wa kuteua Mawaziri na kutengeneza serikali, mfano mzuri wa serikali hii ni serikali ya Austrelia, uingereza na Canada
Katika Parliamentary Government, Bunge lina nguvu kuliko serikali kwa maana kwamba serikali inatengenezwa na chama chenye wabunge wengi Bungeni na hivyo basi mkuu wa serikali ni Waziri mkuu na mda wote anawajibika Bungeni, kwa maana hiyo Wananchi wanawachagua wabunge na wabunge wanaichagua serikali na ndio maana Bunge lina nguvu kuliko serikali.
Kutokana na aina hiyo ya serikali vile vile aina nyingine ya Serikali ni Presindential government system hii ni aina nyingine ya serikali ambayo mkuu wa serikali na nchi ni Rais na ndio anaeongoza shughuli zote za serikali, na mfano wa aina hii ya serikali hii ni serikali ya Marekani na Kenya.
serikali hii hunatumia mfumo wa Individual ministerial Responsibility yaani waziri na Wizara yake wanawajibika Bungeni kwa sababu waziri sio mbunge kwa hiyo anapohitajika bungeni anakuja kuitetea Wizara yake, hili kama mtakumbuka vizuri lilikuwa ni moja wapo la mapendekezo ya Katiba ya wananchi inayotokana na Tume ya Jaji Waryoba
Swali langu Je Serikali ya tanzania haitokani na Bunge na mawaziri sio wabunge?.
Serikali na Bunge yote yana nguvu sawa kwa sababu wabunge na rais wote wanatokana na wananchi kwa hiyo wanawajibika kwa Wananchi vile vile Wabunge wanaweza kumpigia kura ya kutokuwa na imani na Rais na Rais anaweza kulivunja bunge, hii aina Rais anaweza kuwa na wabunge wachache ila akatengeneza Serikali.
Hitimisho Kutokana na kilio cha mda mrefu cha wananchi ili kuwepo na mfumo mzuri unaoeleweka katika serikali yao, ndio maana wananchi wakapendekeza katika tume ya Jaji Waryoba mfumo wa Pure Presidential system, ili kuondokana na katiba ya mwaka 1977 ambayo aina mfumo thabiti, lakini serikali ya ccm imekuwa ikiikumbatia kulinda maslahi ya chama sio nchi.
Ni mimi Mhere Mwita.