Waziri MWAKYEMBE aishauri ICC kufanyia kazi malalamiko ya Afrika

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,495
54,911
Waziri wa Katiba na Sheria Dokta HARISSON MWAKYEMBE ameishauri Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai-ICC kutatua manung`uniko ya Bara la Afrika
image.php

Waziri wa Katiba na Sheria Dokta HARISSON MWAKYEMBE

Waziri wa Katiba na Sheria Dokta HARISSON MWAKYEMBE ameishauri Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai-ICC kutatua manung`uniko ya Bara la Afrika kuhusu viongozi Afrika kutotendewa haki wanapopelekwa katika mahakama hiyo.

Waziri MWAKYEMBE amesema hayo jijini ARUSHA mara baada ya kufungua mkutano ulioandaliwa na mahakama hiyo, ambapo amesema TANZANIA inaunga mkono juhudi za ICC na kuiomba kusikiliza maoni ya viongozi wa Afrika juu ya utendaji wake.

Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Waafrika -PALU DONALD DEYA amesema mahakama ya ICC inapaswa kujiangalia upya hali ili kubaini namna nzuri ya kutenda haki.

Naye Msajili wa Mahakama ya ICC HERMAN VON HEBEL amesisitiza kuwa mahakama hiyo itaendelea kuleta amani, haki na usawa duniani.

Wanasheria wa nchi za Afrika na mashirika ya sheria wamekutana Jijini ARUSHA kuzungumzia masuala kadhaa yanayojitokeza katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai –ICC.

Na SECHELELA KONGOLA
 
Back
Top Bottom