Wana JF,
Itakumbukwa kuwa mwaka 1996 ziliibuliwa tuhuma juu ya aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CCM, Mh. Kihiyo kuwa alikuwa amegushi vyeti na hivyo ukweli juu ya elimu yake ukawa na walakini. Baada ya ufuatiliaji wa karibu na kwa kufuata taratibu za kisheria ilithibitika kuwa alikuwa amegushi na ikapelekea kuvuliwa ubunge na kuleta msamiati 'kihiyo'
Leo hii kuna malumbano juu ya elimu na uwezo wa naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, Mh. Mulugo, hali inayopelekea wengi kuwaza kuwepo mazingira ya kugushi vyeti. Akina Masumbuko Lamwai waliokomaa na Kihiyo mpaka kikaeleweka, leo hii wako wapi? Wapo watu waliosoma na Mh. Mulugo, hebu wajitokeze kuweka mambo wazi ili kuokoa mustakabali wa elimu ya nchi hii ambayo bila kumumunya maneno, hali yake si nzuri hata kidogo.